Wanajeshi wa Kenya wamewashambulia na kuwaua zaidi ya wanamgambo mia moja wa al Shabaab na kuharibu kambi yao nchini Somalia.
Hii ni baada ya wapiganaji wa kundi hilo kulivamia basi moja lililokuwa likisafiri kwenda Nairobi kutoka Mandera na kuwaua abiria 28 kati ya 60 waliokuwemo, wapiganaji hawa waliwalazimisha wasafiri kusoma Qur an, na kumuua kila aliyeshindwa kusoma.
Naibu Rais William Ruto amesema jana kuwa majeshi ya Kenya yalifanya operesheni mbili zilizofanikiwa, ambapo kando na vifo hivyo, pia magari manne yaliyokuwa na silaha yaliharibiwa na kambi yao kuteketezwa.
Lakini kundi la al Shabaab lilijibu haraka na kukanusha madai hayo lililoyataja kuwa yasiyo na msingi wowote. Msemaji wa kijeshi wa kundi hilo Abdulaziz Abu Musab alisema wanamgambo wake hawakukabiliwa na shambulizi lolote baada ya operesheni yao ya Jumamosi.