Wanamgambo wa kundi la Taliban nchini Afghanistan wamedai kuhusika katika mashambulizi yaliyolenga kituo kimoja cha wamishonari wa kikiristo mjini Kabul.
Wanamgambo hao ambao wamesema kuwa hawata ruhusu wamishionari hao wanaojifanya wanatoa msaada na kusambaza fikra zao potofu za kikristo waendee kufanya upotovu huo katika nchi ya kiislamu ya Afghanstan.
Shambulizi hilo lilifonyika katika mtaa wa Karte Seh ni la karibuni kabisa kati ya mfulululizo wa mashambulizi ambayo yamefanywa na kundi hilo wiki hii katika mji huo mkuu wa Afghanistan.Taliban imezidisha mashambulizi huku majeshi ya kigeni yakijiandaa kuondoka nchini humo mwishoni mwa mwezi ujao.Kwingineko nchini humo, maafisa wamesema wanajeshi 11 wa Afghanistan wameuawa katika mashambulizi kusini mwa jimbo la Helmand.Kiasi ya wanamgambo 20 pia wameuawa katika mashambulizi hayo.
Inafaa kuashiria kwamba majeshi ya kigeni yaliivamia Afghanstan kwa lengo la kumsaka Bilionea Osama bin Laden ambaye ni askari mpelelezi wa zamani wa Marekani ambaye pia alituhumiwa kuhusika na shambulio la september 11.