30 Novemba 2014 - 07:32
Watu wawili wameuwawa katika maandamano nchini Misri

Watu wawili wameuwawa katika ghasia kati ya Polisi wa Misri na waandamanaji mjini Cairo baada ya mahakama moja nchini humo kumfutia mashitaka ya mauaji rais wa zamani Dikteta Hosni Mubarak.

Watu wawili wameuwawa katika ghasia kati ya Polisi wa Misri na waandamanaji mjini Cairo baada ya mahakama moja nchini humo kumfutia mashitaka ya mauaji rais wa zamani Dikteta Hosni Mubarak.

 Zaidi ya waandamanaji 1000 walikusanyika katika uwanja wa Tahrir mapema hapo jana, ambapo polisi walitumia mabomba ya maji na gesi ya kutoa machozi kuwatawanya. Mmoja wa waandamanaji aliyekasirishwa na uamuzi huo wa mahakama amesema uamuzi huo hauna haki, na kwamba watu wa Misri hawastahili jambo kama hilo kutoka kwa mahakama hiyo baada ya kungoja uamuzi kwa muda mrefu. Diskteta Hosni Mubarak alikata rufaa dhidi ya kifungo cha maisha alichopewa kwa mauaji ya wanaharakati waliyoipinga serikali, katika maandamano ya kutaka mageuzi yaliofanyika mwaka 2011.  Zaidi ya watu 800 waliuwawa katika maandamano hayo. Rais huyo wa zamani sasa anatumikia kifungo tofauti cha makosa ya ubadhirifu wa fedha za umma, pia anakabiliwa na shtaka la kuuza rasilimali ya gesi kwa utawala wa Israel kwa bei ya chini kuliko bei ya sokoni, jambo ambalo mpaka sasa limewashangaza wamisri wengi kwanini auze gesi kwa utawala wa Israek kwa bei ya hasara ili hali kunawatu wanaohitaji gesi kwa bei ya kawaida na iliyobora.

Tags