3 Januari 2015 - 19:33
Marekani yauwa wapiganaji wa Talibani 18

Wapiganaji kumi na wanane wa Taliban wameuwawa baada ya kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani kusini mwa Afghanistan katika wilaya ya Gayan.

Wapiganaji kumi na wanane wa Taliban wameuwawa baada ya kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani kusini mwa Afghanistan katika wilaya ya Gayan.

Upande wa Taliban haujasema lolote kufuatia shambulizi hilo lililotekea katika eneo linalotajwa kuwa maficho ya wanamgambo hao. Novemba mwaka uliopita mtu aliejitoa mhanga alijiripua katika umati uliokuwa ukiangalia mchezo wa mpira wa mikono na kusababisha vifo vya watu 57 na wengine 60 kujeruhiwa.

Tags