15 Januari 2015 - 19:03

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis amesema kuwa kuna mipaka ya uhuru wa kujieleza, na wala haitakiwi kutusi au kudhihaki imani ya mtu.

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis amesema kuwa kuna mipaka ya uhuru wa kujieleza, na wala haitakiwi kutusi au kudhihaki imani ya mtu.

Papa Mtakatifu Francis amezungumza kuhusu mashambulizi ya kigaidi ya Paris wakati akielekea nchini Ufilipino, akitetea uhuru wa kujieleza siyo tu kama haki ya kimsingi ya binaadamu lakini jukumu la kueleza fikra za mtu kwa ajili ya lengo zuri. Pia Papa Francis, amewaomba viongozi wa Kiislamu kulaani vitendo vya itikadi kali akisisitiza kuwa siyo jambo la kawaida kuuwa katika jina la Mungu na akasema dini haiwezi kutumiwa kuhalalisha vurugu. Kiongozi huyo mkuu wa kanisa katoliki aliwasili leo nchini Ufilipino katika ziara ya siku tano. Papa Francis taongoza misa ya wazi siku ya Jumapili mjini MANILA, ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na watu milioni sita.

Tumekuwa tukishuduhidia magaidi wa Daesh wakiua watu huko Iran na Syria na kufanya jinai kwa kutumia jina la dini ya uislamu, pia tumeona magaidi wa kikristo wa Ant balaka wakiua waislamu wasio na hatia na kuyanasibisha mauaji yao na imani ya kikristo, vile vile tumeshuhudia wafuasi wa dini ya kiyahudi wakiua wapalesatina na wafuasi wa dini ya Buda wakiua waislamu na kunasibisha mauaji hayo na imani za dini zao, kwa kawaida dini ni kitu cha amani, dini haipo kwa ajili ya kuvunja amani.

Kitendo cha kumdhihaki mtume Muhammad s.a.w ni kitendo kinachopingwa na kila mtu mwenye akili timamu, uhuru wa kujieleza haumaanishi kudhalilisha watu, hakuna mtu mwenye uhuru wa kudhalilisha watu, ingekuwani vyema angeanza kujidhalilisha yeye, wazazi wake, familia yake na watu wake wakaribu badala ya kudhalilisha watu watukufu wasio na madoa katika ulimwengu, eti kwa sababu ya kutafuta umaarufu au kutafuta pesa.

Shambulio la Paris lilio ua watu 12 ni shambulio lililosababishwa na waandishi hao wa magazeti waliochupa mipaka ya uhuru, kwa sasa magaidi wameahidi kufanya shambulizi kubwa zaidi je ni nani anafaa kulaumiwa katika mashambulizi kama haya? Je alaumiwe mchokozi au mchokozwa?

 Viongozi wa ulimwengu wameonekana kulikuza sana sambulio liliouwa watu 12 ili hali kuna mashambulizi yanaliyoua mamia ya watu lakini hakuna viongozi wa dunia walio andamana au hata kulaani mauaji hayo, je mauaji mabaya ni mauaji ya Ufaransa tu au mengine pia yanafaa kukemewa?

Ufaransa ni moja kati ya nchi zinayoyaunga mkono makundi ya kigaidi ya yanayopambana Syria kwa ajili ya kuiangusha serikali ya Syria, baada ya makundi hayo kuishambulia Ufaransa sasa yanaonekana ni makundi ya kigaidi lakini mwanzo yalikuwa ni makundi ya wapigania Demokrasia. Umefika  muda kwa ulimwengu kuamka na kuchambua mchele na pumba na si kuendelea kupumbazwa na vyombo vya habari bila ya kufikiria.  

Tags