19 Januari 2015 - 20:44
Ujumbe wa maneno mawili wa Kiongozi wa Hizbollah kwa Israel

Kiongozi wa Hizbullah Sayyid Hasan Nasrullah ametoa ujumbe wa maneno mawili kwa serikali ya Israel kufuatia shambulizi lililofanywa na Israel dhidi ya wanajeshi wa Hizbollah na kuua askari 7, ambapo askari sita ni wa makomando wa Hizbullah na mmoja ni Jenerali wa jeshi la Jamhuri ya kiislamu ya Iran Jeneral Muhammad Ali Alahh Dodii.

Sayyid Hasan Nasrullah amesema maneno mawili tu kuiambia serikali ya Israel kwamba: “Andaeni Pakujificha “. Mwisho wa nukuu.

Kwa sasa viongozi na raia wa Israel wanawasiwasi mkubwa kutokana na kisasi kinachowakabili, inasemekana raia wa mipakani wameanza kuhama kwa woga wa mashambulizi ya makomandoo wa Hizbullah.

Wanajeshi hao wameuawa wakiwa katika ardhi ya Syria ambako wanadumisha amani na kupambana na magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya Syria ambao wanapata msaada kutoka Israel, Marekani na Mataifa ya Ulaya.

Weledi wa mambo wameilaumu sana Israel kwa kuvuka mipaka na kushambulia nchi jirani na kwamba wasilaumu majibu yatakayokuja baada ya uchokozi huo.

Mpaka sasa jeshi la jamhuri ya kiislamu ya Iran ambalo linahesabika kuwa ni moja kati ya majeshi matano yenye nguvu duniani, halijatoa tamko lolote kufatia shambulizi hilo la Israel.

Weledi wa mambo wanasema kuwa maneno ya Sayyid Hasan Nasrullah yanaashiria kutokea tukio la kutisha kwa Israel.

Tags