14 Februari 2015 - 10:37
Hatuwezi maliza mgogoro wa Syria bila Bashar Asad

Suluhisho lolote katika mapigano nchini Syria linapaswa kumuhusisha pia rais Bashar al-Assad, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria amesema katika hatua ya kwanza ya Umoja wa Mataifa kukiri hilo.

Suluhisho lolote katika mapigano nchini Syria linapaswa kumuhusisha pia rais Bashar al-Assad, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria amesema katika hatua ya kwanza ya Umoja wa Mataifa kukiri hilo.

"Rais Assad ni sehemu ya suluhisho," Staffan de Mistura ameuambia mkutano wa waandishi habari pamoja na waziri wa mambo ya kigeni wa Austria Sebastian Kurz mjini Vienna jana Ijumaa tarehe 13 mwezi wa pili mwaka 2015.

"Nitajaribu kuendelea kuwa na majadiliano muhimu pamoja nae," de Mistura ameongeza, akidokeza kwamba "Suluhisho pekee ni la kisiasa."

Hii ni mara ya kwanza kwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria kutamka wazi na kumtaja Assad kuwa sehemu ya suluhisho la amani baada ya miaka karibu minne ya mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi wanaotaka kuuangusha utawala wake.

Matamshi ya de Mistura yamesababisha shutuma kutoka kwa kundi la upinzani la muungano ya kitaifa pamoja na wanaharakati nchini Syria.

"Nafikiri de Mistura anajidanganya mwenyewe iwapo anafikiri kuwa Assad ni sehemu ya suluhisho," mwanachama wa kundi hilo la muungano wa kitaifa Samir Nashar ameliambia shirika la habari la AFP kwa simu kutoka Istanbul.

"Assad ni tatizo, na sio sehemu ya suluhisho."

Najib Ghadbian, mjumbe wa muungano wa kitaifa katika Umoja wa mataifa, ameueleza ukatili wa utawala wa Assad kuwa ndio chanzo cha mzozo huo.

Pia ameuonya muungano unaoongozwa na Marekani unaopambana na kundi lakigaidi la Daesh ambalo kwa jina jingine linajulikana kama kundi  Dola la Kiislamu kundi hili lilikuwa limekamata maeneo makubwa ya ardhi nchini Syria na Iraq na kwamba juhudi zake zinaweza kushindwa hadi pale mataifa yenye nguvu duniani yatakapochukulia kwa dhati mpango ya amani wa syria.

"Tunakaribisha muungano huu lakini tunahitaji kuwa na mkakati maalum kusisitiza sababu ya msingi: Assad na ukatili wa Assad," amesema Ghadbian.

De Mistura, ambaye alikuwa mjini Damascus wiki hii kukutana na Assad, anatarajiwa kutoa ripoti yake kuhusu ujumbe wake katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Februari 17 mwaka huu wa 2015.

Kundi la Daesh ndilo litafaidika na ghasia hizi

Iwapo halitapatikana suluhisho katika mzozo huu, de Mistura amesema "kundi pekee litakalochukua fursa ya mzozo huu ni kundi la  kigaidi la Daesh (Dola la Kiislamu).

Kundi hili ni "zimwi linalosubiri mzozo huu kuanza ili kuweza kuchukua fursa hiyo," amesema.

Lakini Nashar hakubaliani, akisema: "Iwapo Assad kweli alikuwa anataka kupambana na Daesh, angetuma majeshi yake kwenda Raqa badala ya Douma."

Raqa ni mji uliotangazwa na kundi hilo la Dola la Kiislamu kuwa mji mkuu wao kaskazini mwa Syria, wakati Douma ni ngome kuu ya waasi katika eneo la mashariki la Ghouta mashariki mwa Damascus ambao umezingirwa na majeshi ya serikali kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Zaidi ya watu 183 wameuwawa katika mashambulizi ya karibu kila siku mjini Douma katika muda wa wiki chache zilizopita, kwa muijibu wa shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria, ambalo limesema watoto 29 ni miongoni mwa waliouwawa.

"Inaelekea de Mistura hajasikia juu ya mauaji ya kiholela mjini Douma," amesema Nashar.

Mwanaharakati kutoka Douma, ambaye amejitaja kuwa ni Mohammed salaheddin, pia amepinga tathmini hiyo ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa.

"Assad anaweza tu kuchangia katika suluhisho la kisiasa kwa kuyaamuru majeshi yake kusitisha mashambulizi ya makombora dhidi ya raia na kwa -- kuondoa mzingiro katika mji wa mashariki wa Ghouta,"

Lakini wataalam wa mambo ya kijeshi wanasema kwamba kitendo cha jeshi la Syria kuuacha mji wa Ghouta kutapelekea magaidi  hao kuwa na nguvu za kushambulia mji mkuu wa Syria, jambo litakalopelekea  hali ya amani kuwa mbaya zaidi.

Wapambanaji mahili wa Hizbullah pamoja na wanajeshi wa ulinzi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran yapo bega kwa bega na wanajeshi wa Syria katika kupambana na magaidi hao, jambo lilipelekea ndoto za nchi za magharibi na Israel za kuiangusha serikali ya Syria katika kipindi kisichozidi miezi sita, kuwa ni ndoto za alinacha.

Yafaa kuashiria kwamba Marekani, Israel, Ulaya na baadhi ya nchi za kiarabu wamekuwa wakidhamini makundi ya wapambanaji ili kuiangusha serikali ya Bashar Asad, lakini uwezo na utiifu wa jeshi la syria umesabisha kuwashinda maadui zao, ambao mpaka sasa ni miaka minne wameshindwa kufikia malengo yao ya kuiangusha serikali ya Syria.

 

 

Tags