Shirila la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kombora lililorushwa na jeshi la Yemen limelenga kambi ya jeshi nchini Saudia arabia na kusababisha hasara kubwa.
Askari mmoja wa Saudi Arabia na makumi ya askari vibaraka wanaopigana kwa niaba ya Saudia arabia ameuawa na kombora hilo lililofyatuliwa na wanajeshi wa Yemen ambalo lilishambulia kambi ya jeshi iliyoko karibu na eneo la mpaka nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Saudi Arabia kombora hilo lilifyatuliwa jana jioni kutoka katika eneo linalodhibitiwa na wanajeshi wa Yemen na kushambulia kambi hiyo iliyoko katika mji wa Dhahran kusini mwa nchi hiyo na kumuua mwanajeshi wa mpakani Atallah Yassine Al-Anzi pamoja na askari wengi kutoka nchi zinazounga mkono Saudia arabia katika mashambulizi dhidi ya raia wa Yemen.
Kwa miaka miwili Saudi Arabia inayoongoza majeshi ya muungano wa nchi za Ghuba yanayomuunga mkono Rais wa Yemen Abedraabbo Mansour Hadi imefanya mashambulizi ya kinyama dhidi ya wananchi wa Yemen kwa lengo la kumrudhisha madarakani rais huyo ambaye wananchi hawamtaki.
Umoja wa Mataifa ambao umekaa kimya na kutazama mauaji hayo yakiendelea unakadiria kuwa zaidi ya watu wasio ana hatia 7,700 wameuawa nchini Yemen na wengine 40,000 kujeruhiwa tangu mgogoro huo ulipoanza kushika kasi Machi 2015. Umoja wa Mataifa tayari umeonya kuwa Yemen inakabiliwa na hatari ya kukumbwa na njaa mwaka huu.
Mwisho wa habari/ 291