(ABNA24.com) Ayatullah Mohammad Imami Kashani, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ameongeza kuwa: "Wale ambao wamevamia Yemen na Palestina na kuwadondoshea watu mabomu wanataka kuangamiza Ulimwengu wa Kiislamu."
Khatibu wa Sala ya Ijumaa amesisitiza kuwa, wale wanaofanya vitendo hivyo wanauvunjia heshima ulimwengu mzima wa Kiislamu na kuudhalilisha umma wa Kiislamu. Ameongeza kuwa, "Iwapo Waislamu wataungana, basi adui hawezi kuwa na satwa juu yao."
Ayatullah Imami Kashani aidha ameashiria jitihada za utawala wa Kizayuni za kutoa taswira potofu kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga Mayahudi na kusema: "Si Mayahudi wala si Wakristo walio dhidi ya Mwenyezi Mungu bali ni Wazayuni ndio walio dhidi ya Mwenyezi Mungu, dhidi ya ubinadamu na dhidi ya thamani zote."
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuna Mayahudi ambao wanaupinga utawala wa Kizayuni wa Israel na wanaamini kuwa utawala wa Kizayuni ni dhidi ya Mwenyezi Mungu.
Ayatullah Imami Kashani aidha amesema, kuwa macho watu wa Iraq na kuzingatia kwao nasaha za Marajii na viongozi wa kidini kumepelekea kuvunjwa njama za maadui nchini humo. Amesema wananchi wa Iraq wana haki ya kulalamika kuhusu ughali wa maisha na usimamizi mbovu wa nchi lakini malalamiko hayo hayapasi kutumiwa vibaya na maadui.
..........
340