-
Asubuhi ya Qur'an, Hifdhi na Taj'wid katika Hawzat ya Mabanati ya Hazrat Zainab (s) - Kigamboni, Dar-es-salaam
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Asubuhi na Qur'an, katika vipengele vya kuhifadhi, Tajweed, mtiririko mzuri wa damu, kusoma kwa Sauti nzuri, ni zoezi la kila Siku Asubuhi linaloendelea katika Hawzat ya Masista (Mabanati) ya Hazrat Zainab (sa) iliyopo maeneo ya Kigamboni - Dar-es-salaam - Tanzania chini ya Jamiatul Mustafa (s) International Foundation.
-
Washindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel watoa wito wa kukomeshwa mauaji ya kimbari huko Gaza
Washindi wanane wa Tuzo ya Amani ya Nobel wametoa wito wa dharura wa kukomeshwa mara moja mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel huko Gaza na kuhitimisha kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
-
Rais wa Misri kwa mara nyingine apinga kuhamishwa Wapalestina Gaza
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi jana Ijumaa alisisitiza kwa mara nyingine tena kwamba nchi hiyo ya Kiarabu "inapinga kikamilifu" kufurushwa Wapalestina kwenye makazi yao na kuhamishiwa katika nchi nyingine, na kuvitaja vita vya Gaza kuwa "janga la kibinadamu."
-
Ripota Maalumu wa UN: Hali ya kibinadamu Ghaza ni mbaya mno
Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema leo Jumamosi kwamba hali ya kibinadamu huko Ghaza ni mbaya sana.
-
Waziri wa Utamaduni wa Iran anamuwakilishi Rais Pezeshkian katika maziko ya Papa
Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Salehi, yuko Roma ambako anashiriki katika maziko ya aliyekuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, kwa niaba ya Rais Masoud Pezeshkian.
-
Araqchi: Iran iko tayari kupatanisha kati ya India na Pakistan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi ametangaza kwamba Tehran iko tayari "kufanya juhudi za kuzidisha maelewano kati ya India na Pakistan katika kipindi hiki kigumu.
-
Hatua mpya katika kuzidisha kiwango cha ushirikiano kati ya Iran na Russia
Miamala ya kibiashara kati ya Iran na Russia inazidi kuongezeka katika nyanja mbalimbali za kiuchumi hususan katika sekta ya nishati na usafirishaji.
-
Mripuko mkubwa watikisa bandari ya Shahidi Rajaee kusini mwa Iran, 5 wafariki, zaidi ya 500 wajeruhiwa
Mripuko mkubwa umetokea katika bandari ya Shahidi Rajaee kusini mwa Iran na kusababisha uharibifu mkubwa na hasara, huku timu za utoaji huduma za dharura zikikimbilia katika eneo la tukio ili kudhibiti hali hiyo.
-
Trump: Ukraine ndiyo ya kulaumiwa kwa kuanzisha mzozo na Russia
Rais wa Marekani, amedai kuwa maneno yake kuhusu kumaliza vita nchini Ukraine kwa siku moja yalitiwa chumvi, na kusema kuwa Kiev ndiyo ya kulaumiwa kwa kuanzisha vita na Russia.
-
Iran na Marekani zahitimisha duru ya tatu ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana mjini Muscat
Duru ya tatu ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana kati ya wawakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani, ambayo imefanyika Muscat, mji mkuu wa Oman kwa uratibu wa serikali ya nchi hiyo, imemalizika kama ilivyopangwa.
-
Mitihani ya kila Wiki - Hawzat Imam Ridha (as), Burundi
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Katika Picha ni zoezi la Mitihani ya Kila Wiki inayoendelea kila Siku ya Jumamosi katika Hawza ya Imam Ridha (as) - Burundi.
-
Taasisi ya The Desk and Chair Foundation ya Jijini Mwanza chini ya Mwenyekiti wake Alhaj, Dokta Sibtain Megji yatoa Msaada Madawati 100 na Vitu vyake
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Taasisi ya The Desk and Chair Foundation ya Jijini Mwanza chini ya Mwenyekiti wake Alhaj, Dokta Sibtain Megji imetoa msaada wa jumla ya madawati 100 kwa vituo 3 Jijini humo ambapo viti 50 pamoja na Meza zake, vimetolewa katika kituo kimoja huku vingine 50 vikitolewa katika vituo viwili tofauti tofauti. Chanzo: ibnnews
-
Mitihani ya kila Wiki inaendelea kufanyika katika Chuo cha Kisayansi cha Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam - Tanzania + Picha
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa (s) wakiwa katika Mitihani yao ya kila Wiki. Mitihani hii hufanyika kila Siku ya Jumamosi katika Chuo hiki. Ni Mitihani muhimu inayomsaidia Mwanafunzi kujiimarisha zaidi katika masomo yake na kuzidisha uzingativu zaidi katika kile anachofundishwa darasani. Hatua hii humjenga Mwanafunzi na kumuimarisha Kielimu, na hatimaye kuwa Mwanafunzi bora aliyefanikiwa katika masomo yake.
-
Wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa (s) Dar-es-salaam - Tanzania, wakifanya Utafiti wa Kisayansi katika Maktaba ya Chuo Hiki + Picha
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Wanafunzi wa Chuo cha Al-Mustafa International Foundation wakifanya tafiti zao kwenye Maktaba ya Chuo hicho.