26 Aprili 2025 - 22:51
Source: Parstoday
Waziri wa Utamaduni wa Iran anamuwakilishi Rais Pezeshkian katika maziko ya Papa

Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Salehi, yuko Roma ambako anashiriki katika maziko ya aliyekuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, kwa niaba ya Rais Masoud Pezeshkian.

Awali na katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuaga dunia Papa Francis, Rais Pezeshkian alitoa rambirambi na mkono wa pole kwa jamii ya Wakristo duniani kote na wafuasi wa Kanisa Katoliki, na kuashiria juhudi zake za kudumu katika kuhimiza amani, haki, mazungumzo na mshikamano baina dini mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu aidha amepongeza misimamo ya kibinadamu ya Papa Francis hususan hatua zake za kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na kusisitiza kwamba kumbukumbu na jina lake litaendelea kuwepo katika nyoyo za dhamiri zilizoamka na watu wanaopigania uhuru duniani.

Waziri wa Utamaduni wa Iran anamuwakilishi Rais Pezeshkian katika maziko ya Papa

Papa Francis, kiongozi wa Wakatoliki duniani, ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika kukuza mazungumzo kati ya dini mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni, alifariki dunia Jumatatu, 21 Aprili, mjini Vatican akiwa na umri wa miaka 88.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha