Taarifa iliyotolewa na Mpango wa Wanawake wa Nobel imesisitiza kwamba machafuko na ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea kufanywa na Israel si matukio ya sadfa, bali ni sehemu ya kampeni ya kimfumo ya kufuta utambulisho na uwepo wa Wapalestina. Taarifa hiyo imesisitiza tena haki ya watu wa Palestina ya kujitawala na kurejea wakimbizi katika nchi yao.
"Sisi, washindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, tunashuhudia mauaji ya kimbari, maangamizi ya kizazi na uvamizi unaoendelea Palestina. Tunasimama pamoja na watu wa Palestina na tunatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti za kukomesha ukatili huu," imesema taarifa hiyo.
Washindi hao wa Tuzo ya Amani ya Nobel wamesema: Tunalaani mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia, uharibifu wa nyumba na miundombinu, na kupuuzwa sheria za kimataifa.
Tawakkol Karman, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nebel mwaka 2011 amesema: "Mapambano ya wanawake wa Palestina kwa ajili ya kubakia hai na kupata hadhi ya binadamu ni mapambano yetu ya pamoja," na ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuiwekea Israel vikwazo vya silaha.
342/
Your Comment