26 Aprili 2025 - 22:48
Source: Parstoday
Trump: Ukraine ndiyo ya kulaumiwa kwa kuanzisha mzozo na Russia

Rais wa Marekani, amedai kuwa maneno yake kuhusu kumaliza vita nchini Ukraine kwa siku moja yalitiwa chumvi, na kusema kuwa Kiev ndiyo ya kulaumiwa kwa kuanzisha vita na Russia.

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa peninsula ya Crimea itasalia kuwa sehemu ya Russia katika makubaliano ya kutatua mzozo wa Ukraine, na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anaelewa suala hili.

Trump amesisitiza kuwa: Kiev ndiyo ya kulaumiwa kwa kuanzisha mzozo nchini Russia; Sababu ni kwamba Ukraine ilianza kuzungumzia suala la kujiunga na NATO.

Rais wa Marekani amedai kuwa: Mazungumzo ya kutatua mzozo wa Ukraine yanaendelea vyema na makubaliano yanakaribia sana. Rais wa Marekani pia anaamini kuwa inawezekana kupatikana amani nchini Ukraine wakati wa uongozi wake.

Sambamba na kukiri kwamba matamshi yake alipoahidi kumaliza vita nchini Ukraine kwa siku moja yalitiwa chumvi, Trump ameongeza kuwa: "Sidhani kwamba Ukraine itawahi kujiunga na NATO."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha