-
Kuuawa kwa "Mohammad Ali Jamoul", Kamanda wa Kikosi cha Makombora cha Hezbullah katika Shambulio la Ndege Isiyo na Rubani la Utawala wa Kizayuni
Mohammad Ali Jamoul, Kamanda wa kikosi cha Makombora cha Harakati ya Hizbullah, ameuawa Kigaidi kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani (drone) lililofanywa na utawala haram wa Kizayuni (Israel). Shambulio hili linaonekana kuwa sehemu ya mfululizo wa mashambulizi ya Israel dhidi ya viongozi na miundombinu ya Hizbullah.
-
Ripoti ya Picha | Mkutano Mkuu wa Wajumbe wa Ulinganizi na Wahitimu wa Sayansi za Kiislamu wa Niger kwa Kuhudhuriwa na Ayatollah Ramezani + Picha
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mkutano Mkuu wa wajumbe wa ulinganiaji (Mubalighina) na wahitimu wa Sayansi za Kiislamu nchini Niger umefanyika katika Mji wa "Niamey", Mji Mkuu wa nchi hiyo. Mkutano huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya za Kiislamu wa Niger pamoja na Kiongozi wa Tarika ya Tijaniyya nchini humo. Mgeni maalumu wa Mkutano huu alikuwa Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as).
-
Ripoti ya Picha | Hafla ya Kuvalishwa Amama kwa Wanafunzi wa Dini Niger na Ayatollah Ramezani + Picha
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hafla ya kuvalishwa amama kwa kundi la Wanafunzi wa Dini kutoka tawi la Jamiat Al-Mustafa (s) nchini Niger imefanyika kwa kuhudhuriwa Ayatollah Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as).
-
WHO: Matumizi ya tumbaku yanaua watu milioni 6 kila mwaka
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, matumizi ya tumbaku huua takribani watu milioni sita kila mwaka. Watu laki sita kati ya hao, hufa kutokana na kuathiriwa na moshi wa sigara zinazovutwa na watu wengine.
-
UN: Ni "Uhalifu wa Vita" kuzuia chakula kuwafikia Wapalestina wa Gaza
Mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa hatua ya Israel ya kuzuia misaada ya chakula kwa raia wa Palestina walioko kwenye njaa katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa ni uhalifu wa vita, hasa ikiwa inalenga kuwaondoa kwa lazima.
-
Jeffrey Sachs: Marekani bado haikubali ukweli kuwa ubeberu wake umeisha dunaini
Mchumi mashuhuri wa Kimarekani, Profesa Jeffrey Sachs, amesema kuwa enzi ya Marekani kuwa dola kuu duniani imefikia kikomo, lakini Washington bado haijakubali ukweli huo.
-
Barcelona yavunja uhusiano na Israel kutokana na mauaji ya Gaza
Baraza la Jiji la Barcelona limetangaza kuvunja uhusiano wa kitaasisi na utawala wa Israel kutokana na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
Trump amfanyia istihzai Macron kwa kuzabwa kibao na mkewe hadharani
Rais wa Marekani, Donald Trump ameonekana kumfanyia dhihaka mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ambaye hivi karibuni alidhalilishwa na mkewe hadharani.
-
Iran yalalamika kufuatia matamshi ya kichochezi ya Austria kuhusu mpango wa nyuklia
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imemwita Naibu Balozi wa Austria mjini Tehran kulalamikia kile ilichokitaja kuwa ni madai ya “kutowajibika na ya kichochezi” yaliyotolewa na idara ya ujasusi ya ndani ya Austria kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ambao ni wa amani.
-
Iran: Hatutakubali utwishaji wa Magharibi; tutaendelea kurutubisha urani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amepinga vikali mashinikizo ya nchi za Magharibi ya kuitaka Jamhuri ya Kiislamu iache kurutubisha madini ya urani, akiyataja mashinikizo hayo kuwa ni juhudi za kulitwisha taifa la Iran matakwa yao.
-
Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum Atembelea Bunge la Tanzania | Ni Katika Muktadha wa Kukuza Maridhiano na Amani na Maendeleo ya Taifa + Video Fupi
Kwa ujumla, ziara hii imeonesha dhamira ya kweli ya uongozi wa JMAT-TAIFA kushiriki katika mchakato wa maendeleo ya Taifa kwa njia ya ushirikiano na taasisi za kikatiba kama Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.