Jana Ijumaa, baraza hilo lilipiga kura ya kuvunja uhusiano wa kitaasisi na utawala wa Israel na kusitisha makubaliano yake ya urafiki na Tel Aviv "hadi sheria ya kimataifa itakapoheshimiwa na kuhakikishiwa haki za kimsingi za watu wa Palestina."
Uamuzi huo, ambao unajumuisha takriban hatua ishirini, uliungwa mkono na chama tawala cha Kisoshalisti huko Barcelona, vyama kadhaa vya mrengo wa kushoto, na vikundi vinavyounga mkono uhuru.
Hatua hiyo inaashiria kuvunjika kwa uhusiano wa kitaasisi na "serikali ya sasa ya Israel" sanjari na kusitishwa mkataba wa urafiki uliotiwa saini Septemba 24, 1998, kati ya Barcelona na Tel Aviv.
Ikumbukwe kuwa, mwaka 2023, Meya wa jiji la Uhispania la Barcelona alitangaza kusimamisha uhusiano na Tel Aviv kutokana na Israel kukiuka haki za watu wa Palestina kwa njia "iliyoratibiwa". Alitangaza uamuzi huo katika barua yake kwa Waziri Mkuu wa utawala haramu Israel, Benjamin Netanyahu.
Alisema amefikia uamuzi wa kusimamisha uhusiano na Tel Aviv, hadi pale Israel itakapokomesha ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya Wapalestina.
Haya yanajiri siku chache baada ya Jose Manuel Albares, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania kusema kuwa, nchi yake haina nia ya kutoa nasaha kwa yeyote; lakini njia pekee ya kupata amani ni kuitambua nchi ya Palestina, kwani ndiyo njia pekee ya kupatikana amani
Your Comment