Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), amefanya ziara nchini Senegal, iliyoko Afrika Magharibi, kufuatia mwaliko rasmi wa viongozi wa kidini wa nchi hiyo.
Katika ziara hii, inatarajiwa kuwa Ayatollah Ramezani atakutana na wanazuoni, viongozi wa taasisi za Kiislamu, na pia kushiriki katika hafla mbalimbali za kidini na kijamii zinazohusiana na harakati za Ahlul Bayt (a.s) katika eneo hilo.
Katika uwanja wa ndege wa jiji la Dakar, mji mkuu wa Senegal, kikundi cha viongozi wa kidini wa nchi hiyo, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Senegal, mshauri wa masuala ya kitamaduni wa Iran, na mwakilishi wa Jami‘at al-Mustafa nchini humo, walimlaki kwa heshima Ayatollah Reza Ramadhani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s).
Katika safari hii rasmi, Ayatollah Ramezani ameandamana na ujumbe wa ngazi ya juu unaojumuisha:
-
1- Gholamreza Sharifi – Naibu wa Uratibu na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s).
-
2- Dkt. Abdulhossein Kalantari – Mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ahlul Bayt (a.s).
-
3- Hujjatul Islam wal Muslimin Imamzadeh – Mkurugenzi Mkuu wa Nchi za Kiarabu na Kiafrika katika Jumuiya ya Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s).
-
4- Hassan Sadraei Aref – Mkurugenzi na Mhariri Mkuu wa Shirika la Habari la ABNA.
Safari hii inalenga kuimarisha uhusiano wa kidini, kielimu na kitamaduni kati ya jamii ya Waislamu wa Senegal na taasisi za Kiislamu za Iran, hasa kwa kuzingatia mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s).
Inapasa kusemwa kuwa, miongoni mwa shughuli muhimu za Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) katika ziara yake nchini Senegal, ni kukutana na wanazuoni, wasomi, watu mashuhuri wa kitamaduni, pamoja na vijana wa nchi hiyo.
Mikutano hii inalenga kuimarisha mawasiliano ya kielimu na kiroho, kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya umma wa Kiislamu, na kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s) kwa njia ya mazungumzo ya kitamaduni na kijamii.
Your Comment