31 Mei 2025 - 16:41
Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum Atembelea Bunge la Tanzania | Ni Katika Muktadha wa Kukuza Maridhiano na Amani na Maendeleo ya Taifa + Video Fupi

Kwa ujumla, ziara hii imeonesha dhamira ya kweli ya uongozi wa JMAT-TAIFA kushiriki katika mchakato wa maendeleo ya Taifa kwa njia ya ushirikiano na taasisi za kikatiba kama Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa Mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), Samahat Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, amefanya ziara rasmi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Dodoma, Makao Makuu ya nchi.

Katika ziara hiyo, Sheikh Dkt. Alhad aliambatana na ujumbe wake maalum akiwemo Katibu Mkuu Taifa wa Jumuiya hiyo, Askofu Dkt. Gagriel Ole Maasa, ambapo walipokelewa kwa ukaribisho mzuri na wenyeji wa Bunge. Ziara hiyo ililenga kutoa fursa ya kujionea kwa karibu namna vikao vya Bunge vinavyoendeshwa, sambamba na kuelewa kwa undani zaidi michakato ya kisera na kisheria inayochochea maendeleo ya Taifa.

Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum Atembelea Bunge la Tanzania | Ni Katika Muktadha wa Kukuza Maridhiano na Amani na Maendeleo ya Taifa + Video Fupi

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum alieleza kufurahishwa na mwenendo wa vikao vya Bunge na kueleza kuwa ziara kama hizi ni muhimu katika kuimarisha misingi ya Maridhiano na Amani ya Kitaifa, uelewa wa pamoja na ushirikiano katika kujenga Taifa lenye mshikamano.

Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imekuwa mstari wa mbele katika kushajihisha Mazungumzo ya Maridhiano, Amani, Mshikamano wa Kitaifa, na kujenga mazingira ya kuheshimiana kati ya Wananchi wa makundi mbalimbali nchini.

Kwa ujumla, ziara hii imeonesha dhamira ya kweli ya uongozi wa JMAT-TAIFA kushiriki katika mchakato wa maendeleo ya Taifa kwa njia ya ushirikiano na taasisi za kikatiba kama Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum Atembelea Bunge la Tanzania | Ni Katika Muktadha wa Kukuza Maridhiano na Amani na Maendeleo ya Taifa + Video Fupi

Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum Atembelea Bunge la Tanzania | Ni Katika Muktadha wa Kukuza Maridhiano na Amani na Maendeleo ya Taifa + Video Fupi

Your Comment

You are replying to: .
captcha