Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

2 Juni 2023

21:09:40
1370719

Wazayuni wakiri kutokuwa na uwezo wa kuzuia operesheni za wanamuqawama wa Palestina

Operesheni za kishujaa za wanamuqawama wa Palestina zimeongezeka sana na kuvilazimisha vyombo vya habari vya Kizayuni kukiri na kutangaza kuwa Israel imeemewa na haiwezi kukabiliana na operesheni za Wapalestina.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, operesheni ya hivi karibuni ya wanamuqawama wa Palestina karibu na kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha "Haramosh" kaskazini mwa mji wa Tulkarem, na ambayo iliangamiza mlowezi mmoja Mzayuni, imezidisha woga kati ya Wazayuni wakiwemo wataalamu wao wa kijeshi wanaoshindwa kuficha woga na wahka wao hata katika vyombo vya habari vya Kizayuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Shahab, wachambuzi wa masuala ya kijeshi wa utawala wa Kizayuni wanaamini kuwa, kushadidi harakati za muqawama wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni ishara ya kuongeza ujasiri na ushujaa wa wanaoendesha operesheni hizo na wamekuwa wakisema wazi kuwa Tel Aviv haina namna ya kukabiliana na operesheni hizo.

Yossi Yehoshua, mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa gazeti la Kizayuni la Yedioth Aharanot anasema, operesheni za wanamuqawama wa Palestina zinaongezeka na zinazidi kuwa kubwa huku jeshi la Israel likiwa limeshindwa kabisa kukomesha operesheni hizo.

Hillel Rosen, mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa Kanali 14 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni pia amesisitiza kuwa, Israel inalazimika kupeleka vikosi vingi ili kuwatia mbaroni wahusika wa operesheni hizo za Wapalestina na inagharamika sana kutumia teknolojia ya hali ya juu kufanya hivyo.

Rouei Sharon, mchambuzi wa masuala ya Waarabu katika Mtandao wa Kizayuni wa Kan, pia amesisitiza kuwa, jambo la kustaajabisha ni kwamba katika miaka ya nyuma, tulishuhudia ufyatulianaji risasi ukifanyika gizani, kutokea umbali mrefu, na kutumiwa magari kwenye makutano au majumuiko ya watu kama kwenye vituo vya mabasi n.k, lakini katika operesheni za hivi sasa, ujasiri wa wanaoendesha operesheni za ufyatuaji risasi umeongezeka. Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, tumebaini kuwa watu hao wanakwenda hadi karibu kabisa ya magari ya walowezi wa Kizayuni na kuwapiga risasi, bila ya kuviogopa vikosi vya jeshi la Israel.

342/