Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

2 Juni 2023

21:11:00
1370721

WHO: Mlipuko wa Virusi vya Marburg nchini Tanzania umemalizika

Tanzania leo imetangaza mwisho wa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg ambao ulithibitishwa zaidi ya miezi miwili iliyopita katika mkoa wa Kagera kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ya Afrika Mashaariki.

Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo limeelewa kwamba, huo ulikuwa ni mlipuko wa kwanza wa ugonjwa huo nchini Tanzania.

Jumla ya visa tisa na vifo sita vilirekodiwa katika mlipuko huo ambao ulitangazwa mnamo Machi 21 baada ya uchunguzi wa maabara kuthibitisha Marburg ilikuwa chanzo cha vifo na magonjwa ambayo yaliripotiwa katika mkoa huo.

Mamlaka ya kitaifa ya afya kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) na mashirika washirika zilizindua kampeni ya kukabiliana na mlipuko huo ili kukomesha kuenea kwa virusi na kuokoa maisha.

Shirka la Afya Duniani WHO, limekuwa likifanya kazi na nchi tofauti ili kuimarisha utayari na kukabiliana na dharura za kiafya, huku timu za watoa huduma ya kwanza zikifunzwa masuala muhimu ya kujiandaa, kukabiliana na kuzuka kwa mlipuko.

Shukrani kwa juhudi hizi, Tanzania imeweza kukomesha mlipuko huu na kupunguza athari zinazoweza kuwa mbaya za ugonjwa wa kuambukiza," alisema Dk Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, virusi vya Marburg, ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 31 kuambukizwa, saba kati yao walikufa, mnamo 1967 huko Marburg na Frankfurt. Ujerumani na Belgrade huko Serbia.

Ugonjwa wa Marburg husababishwa na virusi vinavyoshabihiana na Ebola na hata dalili zake hazina tofauti kubwa na ugonjwa wa Ebola. Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kikohozi, maumivu ya viungo, kuhara na kutapika, na mara nyingi hata upungufu wa damu katika mwili.

342/