Main Title

source : Parstoday
Jumapili

4 Juni 2023

09:32:38
1371063

Mufti Mkuu wa Belarus: Fikra za Imam Khomeini zimeenea kote duniani

Mufti Mkuu wa Belarus amesema kuwa fikra za Imam Ruhullah Khomeini (RA) zitakumbukwa milele katika historia na ni tochi inayoongoza walimwengu.

Abu Bakr Shabanovich ameyasema hayo katika mkesha wa kukumbuka ya siku ya kuaga dunia mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Ruhullah Khomeini, katika mahojiano maalumu na ripota wa shirika la habari la Iranpress mjini Minsk. Amesema kwamba wakati dhulma, uonevu na ukandamizaji vilipoenea katika jamii ya Iran, Imam alifanya mapinduzi yaliyobadilisha mambo mengi na kuibua mtazamo mpya katika mahusiano ya watu.

Mufti Mkuu wa Belarus amesisitiza kuwa, kwa kawaida mapinduzi huongozwa na shakshia aali zaidi na wasomi, na Mapinduzi ya Kislamu ya Iran yaliongozwa na shakhsia aali na wa juu kabisa yaani Ayatullah Ruhullah Khomeini.

Mufti Shabanovich amesema kuwa Ayatullah Khomeini (RA) alivumilia matatizo mengi kama vile kupelekwa uhamishoni, kukamatwa na kufungwa jela, na ingawa alilazimishwa kuondoka nchini kwake Iran, lakini alifanikiwa kuwaunganisha wananchi kwa ajili ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Mufti Mkuu wa Belarus amesema kuwa Ayatullah Khomeini alikuwa mnadharia mkubwa, na baada ya kurejea nchini kwake akiwa kiongozi mshindi, aliuondoa madarakani utawala wa Shah kwa msaada wa wananchi.

Mufti Mkuu wa Belarus amesisitiza kuwa, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran chini ya uongozi wa Imam Khomeini ni mfano wa kuigwa na Waislamu wote wa Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla ili kujua kwamba kuna ulazima wa kuangamiza tawala za kikoloni kwa ajili ya kujenga nchi yenye msingi wa kanuni za Kiislamu.

Abu Bakr Shabanovich amesema, Imam Khomeini aliwasilisha fikra za Kiislamu kwa ulimwengu kwa namna ambayo fikra hizo sasa zimeuwa za kimataifa na kubakia katika akili za watu wote, na kazi kama hii kubwa hufanywa na watu wakubwa tu.

Akitoa mfano wa fikra adhimu za Imam Khomeini, Mufti Mkuu wa Belarus amesema fikra kama ile ya Siku ya Kimataifa ya Quds kama siku ya umoja wa watu wote na nchi zote za ulimwengu kwa ajili ya uhuru na kujitawala watu wa Palestina sio jambo la sadfa.

342/