Main Title

source : Parstoday
Jumapili

4 Juni 2023

09:35:12
1371066

Mwakilishi wa Syria UN: Kutetea haki za wakimbizi wa Palestina hakuhitaji mjadala

Mwakilishi wa Kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa suala la kutetea haki za wakimbizi wa Kipalestina ni jambo ambalo haliwezi kuwekwa kwenye meza ya mazungumzo kwa ajili ya mjadala.

Bassam al-Sabbagh amesema hayo leo akikosoa masharti yaliyowekwa na Marekani kwa ajili ya kuanza tena kutoa msaada wa dola milioni 300 kwa Wakala wa Umoja wa Mataifa kwa Ajili ya Wapalestina (UNRWA) ili kuwashinikiza Wapalestina wakubaliane na mpango wa kudhalilisha wa Washington ulipewa jina la "Muamala wa Karne".

UNRWA imekuwa ikiwasaidia takriban wakimbizi milioni sita wa Palestina waliokimbia makazi yao katika Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Gaza, Jordan, Lebanon na Syria; na kukatwa kwa msaada huo kumesababisha mgogoro mkubwa wa kifedha kwa shirika hilo. 

Shirika rasmi la habari la Syria (SANA) limeripoti kuwa, akihutubia kikao cha UNRWA mapema leo Jumamosi, Bassam al-Sabbagh amesisitiza msimamo thabiti wa Syria wa kuwaunga mkono watu wa Palestina katika mapambano ya kukomboa nchi yao na ardhi yao iliyoghusubiwa, kwa mujibu wa sheria na maazimio ya kimataifa.

Al-Sabbagh amesema kuwa kadhia ya Palestina ni suala kuu na la kitaifa kwa Syria, na kwamba Damascus haitaacha juhudi zake zote kuunga mkono mapambano ya watu wa Palestina, kukomboa nchi ardhi yao inayokaliwa kwa mabavu na kuunda nchi huru ambayo mji mkuu wake ni Quds tukufu. Mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa nchi hiyo pia itaendeleza jitihada za kuhakikisha kwamba, Palestina inapata uanachama kamili katika umoja huo, na wakimbizi wa Kipalestina wanapata haki yao ya kurejea katika nchi yao iliyoghusubiwa na dola bandia la Israel. 

342/