Main Title

source : Parstoday
Jumapili

4 Juni 2023

09:37:26
1371069

Wanajeshi watatu wa Israel waangamizwa katika mpaka wa Misri

Duru za utawala wa Kizayuni wa Israel zimetangaza kuwa, wanajeshi watatu wa Israel wameangamizwa wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la risasi kwenye mipaka ya Misri na Palestina inayokalia kwa mabavu ambayo imepachikwa jina bandia la Israel

Jeshi la Israel limethibitisha kuwa wanajeshi wake wawili walipigwa risasi na kuuawa karibu na mpaka mapema Jumamosi. Taarifa hiyo imesema  mshambuliaji huyo na mwanajeshi wa tatu wa Israel waliuawa katika makabiliano saa chache baadaye.

Duru za Misri zilisema kundi la watu wenye silaha, pengine 'wasafirishaji wa dawa za kulevya', walishambulia  kituo cha mpakano cha utawala haramu wa Israel kusababisha ufyatulianaji risasi. isasi.

Msemaji mwingine wa jeshi la Israel amesema wanajeshi hao wawili walipigwa risasi wakiwa kazini mapema Jumamosi na miili yao kupatikana baadaye.

Taarifa zaidi zinasema afisa wa polisi wa Misri ndiye aliyewapiga risasi na kuwwangamiza wanajeshi hao wa utawala haramu wa Israel.

Jeshi la  Misri lilithibitisha kwamba mshambuliaji aliyekufa alikuwa mwanachama wa vikosi vya usalama vya Misri.

Tukio hilo la ufyatulianaji risas uliripotiwa katika kivuko cha mpaka cha Nitzana kati ya utawala haramu wa Israel na Misri. Kivuko hicho kiko takriban kilomita 40 (maili 25) kusini mashariki mwa mahali ambapo mpaka huo unakutana naUkanda wa Gaza. Eneo hilo hutumika kuagiza bidhaa kutoka Misri zinazopelekwa Israel au Ukanda wa Gaza.

 

342/