Main Title

source : Parstoday
Jumapili

4 Juni 2023

09:40:05
1371072

Hauli ya mwaka wa 34 tokea alipoaga dunia Imam Khomeini (RA) kufanyika leo

Leo wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wapenda haki kote duniani wanakumbuka mwaka wa 34 tokea alipoaga dunia, Imam Ruhullah Khomeini (RA) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hauli ya mwaka wa 34 tangu alipoaga dunia mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (MA) inafanyika rasmi leo mjini Tehran kuanzia saa mbili asubuhi kwenye haram takatifu ya kiongozi huyo ambapo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei anatazamiwa kuhutubia umma wa wananchi.

Hauli hiyo itaanza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu, tungo za maombolezo na hotuba fupi itakayotolewa na Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Hassan Khomeini, msimamizi wa haram ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, ambaye pia mjukuu wa mtukufu huyo. Baada ya hapo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei atahutubia hadhirina ambapo hotuba yake itarushwa hewani kimataifa moja kwa moja na televisheni za Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama vile Press TV, Al Alam, Al Kauthar na Sahar TV.

Ikumbukwe kuwa, katika siku kama ya leo miaka 34 iliyopita, sawa na tarehe 14 Khordad mwaka 1368 kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Shamsia yaani mwezi Juni 1989, Imam Ruhullah Musawi Khomeini (RA) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliaga dunia akiwa na umri wa 87. Tangazo la kifo cha Imam lilizusha huzuni kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Imam aliongoza harakati za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi tarehe 11 Februari 1979. Mbali na kuwa mwanasiasa shupavu, Imam Khomeini pia alibobea katika taaluma mbalimbali na aliwasomesha wanafunzi wengi na kuandika makumi ya vitabu. Miongoni mwa vitabu vyake ni kile cha Utawala wa Kiislamu na Uongozi wa Faqih.

342/