Main Title

source : Parstoday
Jumanne

6 Juni 2023

20:20:08
1371525

Iran yazindua kombora lake la kwanza la Hypersonic la 'Fattah'

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua kombora lake la kwanza la balistiki la Hypersonic lililopewa jina la 'Fattah'.

Kombora hilo lina uwezo wa kupiga umbali wa kilomita 1,400, sambamba na kutambua na kuharibu ngao za aina zote za makombora.

Rais Ebrahim Raisi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Meja Jenerali Hossein Salami, Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la SEPAH, maafisa wa ngazi za juu serikalini na makamanda wa vikosi vya ulinzi vya Iran wameshiriki katika uzinduzi wa kombora hilo uliofanyika mapema leo katika moja ya kambi za Kikosi cha Anga cha Jeshi la IRGC.

Duru za kijeshi zinaarifu kuwa, makombora ya Hypersonic yana kasi mara tano zaidi ya mwendo wa sauti, na hivyo kuyapa uwezo wa aina yake ya kutoweza kuyatungua.

Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha SEPAH, kombora hilo jipya la balestiki la Hypersonic lililoundwa kikamilifu na wataalamu wa Iran, mbali na kuwa na uwezo wa kupenya kwenye mifumo ya kisasa ya kutungua makombora, lakini lina uwezo mkubwa wa kupiga shabaha kwa usahihi mkubwa.

Anasisitiza kuwa, kombora hilo lina kasi kubwa na uwezo wa aina yake, na hakuna teknolojia yoyote duniani inayoweza kulitungua hata katika kipindi cha miongo kadhaa ijayo.

Hapo jana, Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani, Waziri wa Ulinzi wa Iran alisema sekta ya viwanda vya Wizara ya Ulinzi ya Iran ina uwezo wa kuunda silaha za aina zozote zinazohitajika na vikosi vya ulinzi vya nchi hii.

Mafanikio ya viwanda vya silaha vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hususan katika kuunda makombora ya balistiki katika miaka ya karibuni yamekuwa ya kustaajabisha, jambo ambalo linayatia tumbojoto madola ya Magharibi. 

Kombora la balistiki la Fattah limezinduliwa siku chache baada ya kombora la Khorramshahr 4 lililopewa jina la 'Khaibar' kuzinduliwa rasmi kama bidhaa mpya kabisa ya makombora yaliyoundwa na sekta ya viwanda vya Wizara ya Ulinzi ya Iran, kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kukombolewa mji wa Khorramshahr tarehe 3 Khordad. 

342/