Main Title

source : Parstoday
Jumanne

6 Juni 2023

20:25:18
1371527

Iraq yavunja mtandao wa mabaki ya ISIS mkoani Al-Anbar

Vyombo vya usalama nchini Iraq vimefanikiwa kusambaratisha mtandao wa mabaki ya wanachama wa kundi la kigaidi la ISIS katika mkoa wa Al-Anbar, wa magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu.

Qasim Mosleh, Kamanda wa Jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq la Hashdu-Shaabi amesema wanamapambano wa harakati hiyo ya wanamuqawa wameshambulia ngome na maficho ya mabaki ya wanachama wa magenge ya kigaidi na kuwapa kipigo kikali. 

Amesema kuwa, operesheni hiyo ya kijeshi ya Harakati ya Hashdu Shaabi kwa ushirikiano na kamandi ya operesheni ya mkoa wa Al-Anbar na vitengo vingine vya mapambano dhidi ya ugaidi, imefanikiwa kuvunja mtandao wa genge la ISIS karibu na mipaka ya pamoja na kimataifa na Syria. 

Naye Abdul Wahab Al-Saadi, Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Ugaidi cha Iraq amesema magaidi kadhaa wameangamizwa katika operesheni hiyo iliyofanyika katika mkoa wa al-Anbar.

Mkoa wa Anbar uliokuwa ukidhibitiwa na ISIS ulikombolewa na wanamuqawama

Operesheni za kuwakabili mabaki ya wafuasi waliotawanyika huku na kule wa kundi la Daesh zimeshadidi katika miezi ya karibuni nchini Iraq, hasa katika mikoa ya Nainawa, al-Anbar, Salahuddin pamoja na maeneo mengine ya nchi hiyo yaliyokombolewa kutoka kwenye makucha ya kundi hilo la kitakfiri.

Wananchi wengi na makundi mbalimbali ya nchi hiyo wanaamini kuwa, kuongezeka kwa harakati za Daesh ni matokeo ya njama ya Marekani nchini Iraq inayolitumia suala hilo ili iweze kubaki na kuendelea kuikalia kwa mabavu ardhi ya nchi hiyo.

342/