Main Title

source : Parstoday
Jumanne

6 Juni 2023

20:25:40
1371528

Safari ya al-Miqdad nchini Iraq na kuimarishwa ushirikiano wa kiusalama, kisiasa na kiuchumi

Faisal al-Miqdad, Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, amekutana na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Hussein katika safari aliyofanya mjini Baghdad, ambapo pande hizo zimesisitiza juu ya kupanuliwa uhusiano wa pande mbili hususan kuhusu usalama.

Faisal al-Miqdad aliwasili mjini Baghdad Jumamosi usiku. Ahmad al-Sahaf, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq amesema, al-Miqdad imekutana na waziri mwenzake wa Iraq Fouad Hussein, Rais wa Iraq na Spika wa bunge, Waziri Mkuu pamoja na Mkuu wa Baraza Kuu la Mahakama la nchi hiyo.

Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq nchini Syria ina umuhimu mkubwa kwa kuzingatia nafasi ya nchi hizo katika eneo. Iraq na Syria zina mpaka mrefu wa pamoja wa kijiografia, ambao umekuwa sababu ya ushirikiano kati ya nchi hizo na wakati huo huo chanzo cha wasiwasi kwa Damascus na Baghdad. Fuad Hussein alisema Jumapili katika mkutano na Faisal al-Miqdad kwamba hali ya usalama nchini Syria inaathiri moja kwa moja mambo ya ndani ya Iraq.

Katika miaka ya hivi karibuni, Iraq na Syria zimekabiliwa na tishio la kawaida la ugaidi na bado zinakabiliwa na tatizo hilo. Katika miaka ya nyuma, makundi ya kigaidi yaliteka sehemu kubwa ya ardhi ya Syria na Iraq na kuzisababishia hasara kubwa za kimaada na kibinadamu. Kutokana na mipaka ya pamoja ya nchi hizo mbili na udhaifu wa kiusalama uliopo katika nchi hizo, magaidi wanaweza kuingia kirahisi Iraq kutokea Syria na kuingia Syria kutokea Iraq. Ni kwa kuzingatia ukweli huo ndipo Iraq na Syria zikashirikiana kupambana na ugaidi kwa lengo la kurudisha usalama wa kutosha katika mipaka yao.

Kwa kuzingatia kuendelea kuwepo magaidi katika ardhi ya Syria na mabaki ya Daesh nchini Iraq, bado kuna wasiwasi mkubwa katika pande mbili kuhusu uharibifu unaoweza kufanywa na magaidi hao kwa madhara ya maslahi ya mataifa hayo. Kuhusiana na hilo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq, Ahmad al-Sahaf amesema: Iraq na Syria zinataka kuongeza juhudi za pande mbili kwa ajili ya kudhibiti kwa pamoja mipaka ya nchi hizi, kuzuia kupenya magaidi na kubadilishana taarifa kwa ajili ya kudumisha usalama na utulivu katika mipaka."

342/