Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

23 Februari 2024

16:28:54
1439820

Kuwaunga mkono wananchi na muqawama wa Ghazza ndilo jukumu kubwa la kiQur'ani leo hii

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran amesisitiza kuwa, kuwaunga mkono na kuwasaidia wananchi na muqawama wa Ukanda wa Ghazza ndilo jukumu kubwa zaidi la kiQur'ani hivi sasa.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo Alkhamisi wakati alipoonana na washiriki wa Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaliyofanyika hapa Tehran na kuongeza kuwa, mafundisho ya Qur'ani Tukufu yanatuwajibisha kuwatendea wema wanadamu wengine na kuzisaidia jamii za wanadamu.

Amewalaumu viongozi wa nchi za Kiislamu kwa kushindwa kutekeleza kivitendo mafundisho ya Qur'ani Tukkufu kuhusu Palestina na kusema kuwa, leo hii vikosi vya muqawama huko Ghazza vimesimama kidete kupambana na adui khabithi Mzayuni. Wanafanya hivyo ili kutekeleza kivitendo mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kwa taufiki ya Allah, ushindi utakuwa ni wa taifa la Palestina.Ameongeza kuwa, bila ya shaka yoyote Ulimwengu wa Kiislamu utashuhudia kwa macho yake namna donda ndugu la kensa la Kizayuni linavyoangamia. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, suala la Ghazza ndiyo kadhia kubwa ya Ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu atakwenda kuwauliza wananchi Waislamu ambao wameshindwa kuwashinikiza viongozi wao, kama ambavyo viongozi wa nchi za Waislamu nao watakwenda kuulizwa kwa nini walishindwa kutekeleza mafundisho ya Qur'ani Tukufu kuhusu Ghazza. Aidha amesema, leo hii Ulimwengu wa Kiislamu na watu huru duniani wanaomboleza mateso wanayoyapata watu wa Ghazza. Amesisitiza kuwa, wananchi wa Ghazza wanadhulumiwa na watu ambao hawana chembe ya ubinadamu, ndio maana jukumu kubwa la kila mtu hivi sasa ni kuwasaidia na kuwaunga mkono wananchi madhlumu lakini mashujaa wa Ghazza na muqawama wao.

342/