Pezeshkian ameandika ujumbe maalumu kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X ya mjibizo dhidi ya kukaribishwa na kuhutubia Benjamin Netanyahu katika Bunge la Marekani la Kongresi, na kueleza kwamba "si jinai ya kuua watu wasio na hatia na watoto wasio na pa kukimbilia inaweza kufumbiwa macho, wala si mhalifu anaweza kutakaswa kwa kushangiliwa".Katika ujumbe wake huo, rais mteule wa Iran amenukuu pia aya ya 227 ya Suratu-Shuaraa isemayo: "...Na wanaodhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka". Licha ya maandamano ya umma nchini Marekani ya kupinga kukaribishwa Netanyahu katika nchi hiyo, wajumbe wa Kongresi walisimama mara kadhaa na kumpigia makofi mhalifu na mtenda jinai huyo za kivita wakati alipohutubia bunge hilo.
Katika hotuba yake hiyo iliyojaa madai chungu nzima ya uwongo, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni hakuashiria chochote kuhusu hali mbaya ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, na badala yake alizusha madai yasiyo na msingi wowote kuhusiana na Iran na taifa la Palestina.
Jinai za utawala wa Kizayuni zingali zinaendelea katika Ukanda wa Ghaza, ambapo kwa mujibu wa takwimu za hivi punde, tangu Oktoba 7 hadi sasa zaidi ya Wapalestina 39,000 wameshauawa shahidi na wengine zaidi ya 89,000 wamejeruhiwa.../