Amesema kuwa “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, tumetembelea familia za wakimbizi wa Lebanon waliokuja Karbala, ili kusikiliza mahitaji yao na kuwapa msaada wa lazima kwao”.
Akaongeza kuwa “Ziara hii ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Hussein Sistani, aliyehimiza kusaidia watu wa Lebanon baada ya kushambuliwa na mazayuni”.
Muheshimiwa katibu mkuu amesema “Atabatu Abbasiyya imeunda kamati maalum ya kuhudumia wakimbizi, kuanzia kuwapokea, kuwaandalia sehemu za kukaa, kuwapa chakula na tiba, sambamba na kutuma ujumbe wa watoa misaada kwa wakimbizi wa Lebanon nchini Siria, ikiwa ni pamoja na kugharamia matibabu yao”.
Atabatu Abbasiyya imeandaa majengo maalum kwa ajili ya kupokea wakimbizi, wameandaliwa sehemu za kukaa, chakula, maji, huduma za afya na ushauri wa kisaikolojia.
Atabatu Abbasiyya imetuma shehena tatu zenye maelfu ya tani za misaada ya chakula na tiba, pamoja na kuandaa kituo cha afya na gari za kutoa huduma za tiba, aidha imeandaa jiko maalum kwa ajili ya kupika chakula na kukigawa kwa wakimbizi katika miji iliyoathirika na vita.
alkafeel





