Main Title

source :
Alhamisi

5 Desemba 2013

20:30:00
486419

Historia ya Mandela

Nelson Mandela alizaliwa katika kijiji kimoja kiitwacho, Mvezo katika mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini tarehe 18 Julai mwaka 1918. Alikuwa mtu wa kwanza katika familia yake kwenda shule. Mwalimu ambaye hata hangeweza kutaja jina lake vyema, alizoea kumuita Nelson. Alitoroka mjini Johannesburg mwaka 1941 ili kuepuka kulazimishwa kuoa mapema. Alikutana na Walter Sisulu aliyemsaidia kupata kazi katika kampuni ya ya Witkin Sidelsky na Eidelma. Pia alijiunga na chama cha (ANC)

Kesi ya Uhaini:Mandela alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza ya sheria inayomilikiwa na mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa ushirikiano na Oliver Tambo, na kutoa huduma za kisheria kwa wale ambao walikosa uwakilishi. Akihofiwa kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi wa rangi, ANC ilimtaka Mandela kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza kuendesha harakati zake kimya kimya. Alikamatwa mwaka 1956 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini yeye pamoja na wenzake 155. Baada ya kesi yake iliyochukua miaka minne, ilitupiliwa mbali . Mnamo mwaka 1958, Mandela alimuoa Winnie Madikizela.Kifungo cha Maisha:Sheria ya hali ya hatari ilitangazwa baada ya polisi kuwaua waandamanaji 69 mjini Sharpville mwaka 1960. Serikali ilihofia kuwa wangelipiza kisasi na hivyo kuharamisha chama cha ANC. Chama hicho baadaye kiliendesha harakati zake za kijeshi kichinichini wakiongozwa na Mandela.Mwaka 1962, Mandela alikamatwa kwa kosa la kuondoka nchini bila kibali. Wanachama wengine wa ANC walikamatwa. Akiwa jela Mandela alishtakiwa kwa kosa la hujuma. Yeye na wengine saba walihukumiwa jela katika kisiwa cha Robben mwaka 1964 Kuachiwa huru:Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa mwaka 1967.Shinikizo zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, rais FW De Klerk akakiondolea marufuku chama cha ANC. Tarehe 11 Februari, Mandela aliachiliwa baada ya miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku yeye pamoja na mkewe wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza wa chama cha ANC mwaka uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa chama .Mazungumzo yakaanza ya kuunda serikali ya pamoja ya waafrika weusi na wazungu. Mandela alikuwa karibu sana na rais wa zamani wa Tanzania Julius Nyerere, ambapo serikali ya Tanzania ilitoa msaada mkubwa sana katika kupatikana uhuru wa Afrika kusini. Kuwa Rais:Mnamo mwaka1994,kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, watu wa rangi zote walipiga kura katika uchaguzi huru na wa kidemokrasia. Mandela alichaguliwa. Akihutubia umma, katika sherehe ya kuapishwa kwake, tarehe 10 mwezi Mei, mwaka 1994, alisema: "uhuru utawale, Mungu aibariki Afrika!' Tatizo lake kubwa lilikuwa ukosefu wa nyumba za kutosha kwa watu maskini na mitaa ya mabanda iliendelea kuongezeka.Thabo Mbeki alichukua uongozi wa nchi huku Mandela akiuza sera za nchi hiyo kimataifa.Nelson Mandela alizuru kisiwa cha Robben mwezi Februari mwaka 1995 alikozuiliwa kwa miaka 18. Ziara yake ilikuwa mwaka 1956 mwezi Februari pamoja na wafungwa wenzake waliowahi kufungwa kisiwani humo na kufanya kazi ngumu. Mapafu ya Mandela yanasemekana kuathirika alipokuwa anafanya kazi katika machimbo ya mawe.Thabo Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela kama kiongozi wa chama tawala ANC na hata kushinda uchaguzi wa mwaka 1999.Mandela alimuoa Graca Machel, mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji, akiwa na miaka 80. Aligunduliwa kuwa na saratani ya Tezi Kibofu na hivyo kuanza matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu, akisema kuwa anataka maisha ya kimya nyumbani kwake na familia yake.Kufariki:Mandela aliweza kuonekana hadharani mara kadhaa baada ya kustaafu. Ingawa alionekana katika sherehe ya kukamilika kwa dimba la kombe la dunia mwaka 2010 nchini humo. Januari mwaka 2011, alilazwa hospitalini kwa ukaguzi maalum, huku serikali ikiwakumbusha watu kuwa aliwahi kupata matatizo ya kupumua. Alipokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu mwaka 2012 na pia mwaka 2013 .Mandera amefariki jana tarehe 5 Desemba 2013 Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95, Mandela  aliiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.Mandela amefariki baada ya kusumbuliwa na  homa ya mapafu, amefariki akiwa  nyumbani kwake katika jiji la Johannesburg Afrika kusini,baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.