Gharib-abadi
-
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Marekani Haiwezi Kujitenga na Wajibu Wake Katika Jinai za Kivita
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa, Kazem Gharibabadi, amesema matukio yaliyotokea katika miji ya Minab na Lamerd, kusini mwa Iran, yalikuwa jinai za wazi za kivita, na si makosa ya kiutendaji.
-
Iran: Njia ya muda ya kupitisha meli katika Mlango wa Hormuz imekubaliwa na Oman
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, amesema Iran na Oman zimekubaliana kuhusu njia ya muda ya kupitisha meli katika Mlango wa Hormuz, yenye upana wa maili 7. Amesema ufunguaji kamili wa mlango huo utategemea masharti na mipangilio itakayowekwa na Iran, huku akisisitiza kuwa Tehran bado iko katika hali ya vita.
-
Gharibabadi: Dhana potofu ya Trump kuhusu Mlango wa Hormuz itasahihishwa hivi karibuni
Iran: Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya Kisheria na Kimataifa, Kazem Gharibabadi, amejibu hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuchapisha ramani inayoonyesha Mlango wa Hormuz kama “ardhi mpya ya Marekani”, akisema kuwa “dhana potofu ya Trump kuhusu Mlango wa Hormuz itasahihishwa hivi karibuni.”
-
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Kulinda Bahari ya Caspian ni Jukumu la Pamoja la Nchi Zinazoizunguka
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa, Kazem Gharibabadi, amesema usalama na ulinzi wa Bahari ya Caspian ni jukumu la pamoja la nchi zote tano zinazoizunguka, akionya kuhusu athari za kushuka kwa kina cha maji, uchafuzi na mabadiliko ya tabianchi.
-
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Makubaliano na Oman Hayamaanishi Kufunguliwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, amesema makubaliano kati ya Iran na Oman kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz hayamaanishi kufunguliwa kwa njia hiyo ya kimkakati, akisisitiza kuwa masuala ya Hormuz yatajadiliwa na kuamuliwa na Tehran na Muscat pekee.
-
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Aikosoa Australia kwa Kuwachukulia Hatua Madaktari Wanaoikosoa Israel
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa, Kazem Gharibabadi, amesema hatua dhidi ya madaktari nchini Australia wanaokosoa Israel ni shambulio dhidi ya uhuru wa kujieleza na dhamira ya taaluma ya tiba.
-
Gharib Abadi: Nguvu za Kijeshi za Iran Zililazimisha Adui Kuketi Mezani; Hati ya Mwisho ya Makubaliano Yakamilika
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Gharib Abadi, amesema nguvu za kijeshi za Iran ndizo zilizomlazimisha adui kurejea kwenye mazungumzo, akisisitiza kuwa maandishi ya mwisho ya hati ya maelewano yamekamilika na kutiwa saini rasmi kutafanyika Ijumaa nchini Uswisi, huku Iran ikiahidi kujibu hatua yoyote ya kutotekelezwa kwa ahadi za upande wa pili.