Hekima
-
Imamu wa Ijumaa wa Michigan:Dunia imejifunza kutokana na uongozi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi /Ushindi wa kuvutia wa Iran katika vita vya siku 12
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Basim Al-Shar’i amesema kuwa hatari kuu kwa Jamhuri ya Kiislamuinatokana na mambo ya ndani, na akaongeza: “Nguvu ya wananchi wa Iran imo katika umoja wao na kushikamana kwao na uongozi wenye busara wa Ayatullah Khamenei. Umoja huu ndio heshima na mtaji halisi wa Jamhuri ya Kiislamu.”
-
Dkt. Pezeshkian katika Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Oman:
Iran na Oman zimekuwa zikisaidiana daima katika nyakati za mivutano ya eneo
Hamad bin Faisal Al-Busaidi alielezea furaha yake kwa ziara yake nchini Iran na kukutana na Rais Pezeshkian, akisema kuwa uhusiano wa Iran na Oman ni wa kipekee, wa kihistoria, wa kina na wa ukweli, usio na mashaka. yoyote.
-
Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi:
“Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimewapiga maadui zao Kofi lisilosahaulika”
Jenerali Mousavi alisema kuwa kipindi cha masomo ya kijeshi kwa wanafunzi hao kilitokea katika wakati wa kipekee - wakati ambao muqawama ulithibitisha ushindi wa imani juu ya dhulma na ubabe wa kimataifa.
-
Shia wa Ahlul-Bayt (as) Kamwe Hawatukani Masahaba wala Mtu yeyote hata kama ni dhalimu, bali Hufuata Manhaj wa Qur’an Tukufu katika Kukosoa kwa Hekima
Shia na Mtazamo wao kwa Masahaba Shia hawawatusi Masahaba wa Mtume (s.a.w.w), bali hukosoa matendo au maneno ya baadhi yao pale yanapopingana na mafundisho ya Uislamu na Qur’an Tukufu. Kukosoa kwao si kutokana na chuki, bali ni kutokana na ufuasi wa haki na uchambuzi wa kielimu.
-
Shukrani za Balozi wa Iran kwa Marjaa, Serikali na Wananchi wa Iraq kwa Kufanikisha Maadhimisho ya Arubaini
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Iraq, Bw. Muhammad Kazim Al-Sadiq, ametuma tamko maalum la shukrani kwa Marjaa wa kidini, serikali, wananchi, hasa makabila, vijana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Iraq kwa kufanikisha maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s).