Majlisi
-
Vijana wa Hilali Nyekundu wa Gilan Waadhimisha Maombolezo ya Muharram kwa Hotuba ya Ayatullah Ramadhani mjini Rasht
Maadhimisho ya maombolezo ya siku kumi za kwanza za mwezi wa Muharram kwa vijana wanachama wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Mkoa wa Gilan yamefanyika mjini Rasht, ambapo Ayatullah Ramadhani alisisitiza umuhimu wa kueneza mafundisho na ujumbe wa Mapinduzi ya Ashura.
-
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Iran Waomboleza Tasu'a ya Imam Hussein (a.s.) nchini Mexico
Wachezaji na viongozi wa msafara wa Timu ya Taifa ya Soka ya Iran wamefanya majlisi ya maombolezo ya Tasu'a ya Imam Hussein (a.s.) katika makazi yao mjini Tijuana, Mexico, wakikumbuka mashahidi wa Karbala na kuonyesha mapenzi yao kwa Ahlul-Bayt (a.s.).
-
Majlisi ya Maombolezo ya Muharram Yafanyika Jamiat Al-Mustafa, Dar es Salaam
Majlisi ya maombolezo ya mwezi wa Muharram imefanyika katika Jamiat Al-Mustafa, Dar es Salaam, Tanzania, ambapo mhadhiri alikuwa Sheikh Taqee Zacharia Athumani, akizungumzia sababu za kuhuishwa kwa kumbukumbu ya Karbala kila mwaka.
-
Majlisi ya kuhuisha kumbukumbu ya Imam Hussein (a.s) katika Shule ya Wasichana ya Bibi Zaynab (s.a) – Kigamboni, Dar es Salaam
Katika shule ya wasichana ya Shule ya Bibi Zaynab (sa) kumefanyika hafla ya kuhuisha kumbukumbu ya Imam Hussein (a.s) kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa Ashura na kuelimisha nafasi ya mwanamke katika Uislamu.
-
Muharram 1448H: Wanafunzi Mabinti wa Jamiatul Mustafa Washiriki Majlisi ya Maombolezo katika Msikiti wa Amirul Muuminin (AS), Magomeni
Wanafunzi 144 wa Jamiatul Mustafa, wakiongozana na msimamizi wao, walishiriki majlisi ya maombolezo ya Muharram katika Msikiti wa Amirul Muuminin (AS) uliopo Mgomeni, Dar es Salaam. Majlisi hiyo ilijumuisha muhadhara wa Sheikh Hujjatul Islam wal-Muslimin Aydarus, kisomo cha Qur'ani Tukufu na maombolezo ya Imam Hussein (AS), ikiwa ni sehemu ya kuhuisha ujumbe wa Karbala wa haki, uadilifu na kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu.