Matarajio
-
Araghchi: Tunatarajia OIC Ichukue Nafasi Madhubuti katika Kutatua Changamoto za Ulimwengu wa Kiislamu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araghchi, amesisitiza matarajio ya Iran kwamba Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) itatekeleza jukumu madhubuti katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia ya Kiislamu. Amesema mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa OIC uliofanyika nchini Iraq ulikuwa na umuhimu mkubwa, ukiwa wa kwanza kufanyika nchini humo katika kipindi cha miaka 45.
-
Kivuli cha vita chautanda uchumi wa Ghuba ya Uajemi: Kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta na kudorora kwa matarajio ya ukuaji wa uchumi
Kuongezeka kwa vita na mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati na viwanja vya ndege vya Saudi Arabia kumeweka shinikizo kwenye masoko ya mafuta na hisa katika nchi za Kiarabu zinazopakana na Ghuba ya Uajemi.
-
Wakati mwingine Kukimbizana Zaidi Hukufanya Upoteze Zaidi!
Imam Ali (a.s.) kuhusu kuwa na kiasi katika kutafuta riziki amesema: “Jua kwa yakini kwamba kamwe hutayafikia matamanio yako yote, na [pia jua kwamba] kamwe hutavuka muda wa maisha yako uliopangiwa [wala hutaishi zaidi ya muda uliokadiriwa kwa ajili yako]. Na wewe upo katika njia ileile ambayo waliotangulia walikuwa nayo [wao wameondoka na wewe pia utaondoka]. Kwa kuwa hali ni hiyo, basi usifanye kupita kiasi katika kuitafuta dunia, na katika kazi na kujitafutia kipato uwe na kiasi. Kwa sababu mara nyingi juhudi kubwa [katika kuitafuta dunia] hupelekea mali kuangamia. Zaidi ya hayo, si kila anayejitahidi sana amepata riziki, wala si kila mwenye kiasi amenyimwa. Basi kuweni na kiasi katika kuitafuta dunia; kwa sababu kila mtu atapewa kile alichokadiriwa kwa ajili yake.”
-
Riziki Bila Kudai Fadhila; Kutoka Chanzo Kimoja Pekee
Mwenyezi Mungu ametajwa katika Qur’ani Tukufu kuwa ni “Mbora wa Watoaji wa Riziki.” Riziki ambazo watu huwapa wengine zimechanganyika na mapungufu mengi; ni zenye mipaka na za muda mfupi, na hakuna uhakika wa kuendelea kwake katika siku zijazo. Wakati mwingine huambatana na kudai fadhila, na wakati mwingine huambatana na kumdhalilisha anayepokea au kutarajia malipo ya aina fulani kwa kile alichotoa. Hali ni tofauti na riziki ya Mwenyezi Mungu; haina mipaka wala ukomo, hakuna hofu kuhusu mustakabali wake, wala haina kudai fadhila au matarajio ya malipo. Bali, mwanadamu hupewa riziki tangu anapowekwa tumboni mwa mama yake hadi katika dakika ya mwisho ya maisha yake. Na hata Siku ya Kiyama, riziki hiyo itaendelea kuwepo kwa watu wanaostahiki, katika kiwango cha juu na kilicho bora zaidi.
-
Qalibaf: Ushiriki wa Wananchi kwa Usiku 200 Umevunja Ndoto za Wavamizi, Sio Utashi wa Wairani
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema uwepo wa wananchi katika mitaa kwa muda wa usiku 200 umeonyesha kuwa mashambulizi na shinikizo haviwezi kuvunja dhamira ya watu wa Iran wala mshikamano wao na nchi yao.
-
Rais Pezeshkian: Juhudi za Pakistan za Kuimarisha Amani Zimejikita Katika Utamaduni Wake Tajiri
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema kuwa juhudi za Pakistan katika kuimarisha amani katika eneo la Mashariki ya Kati na Asia zina mizizi katika utamaduni wake tajiri, akisisitiza uhusiano wa karibu na malengo ya pamoja kati ya Tehran na Islamabad.