Teknolojia
-
Mufti Awataka Watanzania Kutumia Teknolojia kwa Maendeleo, Siyo Kuvuruga Amani na Utulivu nchini +Picha
Mufti awataka Watanzania kutumia elimu na teknolojia kujenga nchi na kuleta maendeleo.Akemea matumizi mabaya ya mitandao kuvuruga amani na kuvunja heshima za watu na viongozi. Awataka vijana kuwa makini na watu wanaotumia teknolojia kueneza kashfa na dharau. Asisitiza umuhimu wa kulinda umoja, utulivu na mshikamano wa Watanzania.
-
Waziri wa Sayansi wa Iran Aelekea Riyadh Kushiriki Mkutano wa UNESCO Kuhusu Akili Bandia
Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran, Hossein Simaei, ameondoka Tehran kuelekea Riyadh akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu kwa ajili ya kushiriki mkutano wa UNESCO kuhusu akili bandia (AI).
-
Admirali Sayyari: Iran Imesimama Imara Dhidi ya Adui Mwenye Teknolojia Zote za Dunia
Admirali Habibullah Sayyari amesema Iran inaendelea kusimama imara dhidi ya adui mwenye vifaa na teknolojia zote za kisasa duniani, akisisitiza kuwa vita vya leo ni vita vya utashi na ustahimilivu, si suala la vifaa pekee.
-
Yaliyofichika kuhusu mwenendo wa kielimu na kiutendaji wa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei
Umahiri katika elimu ya fiqhi na masomo ya Hawza, uanzishaji na usimamizi wa vituo vya kielimu, uelewa mpana wa sayansi na teknolojia za kisasa, tafiti za kimkakati katika nyanja mbalimbali, pamoja na kuanzisha mitandao ya taasisi za hisani kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji, ni miongoni mwa mambo ambayo hayajulikani sana kuhusu mwenendo wa kielimu na kiutendaji wa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei.
-
Iran: Baadhi ya Mabomu Yalikuwa Yametengenezwa Maalum kwa Ajili ya Kuishambulia Iran
Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Ibn al-Ridha, amesema adui alitumia mchanganyiko wa zana za kijeshi, mtandao, vikosi vya vibaraka na wapinzani wa ndani katika vita dhidi ya Iran, huku baadhi ya silaha zikitumiwa kwa mara ya kwanza na baadhi ya mabomu yakitengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuishambulia Iran.
-
Aref: Iran Kulenga Kuwa Miongoni mwa Nchi 10 Bora Duniani kwa Akili Bandia na Kushikilia Haki Zake katika Mlango wa Hormuz
Iran: Naibu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref, amesema teknolojia zinazoibukia na akili bandia si chaguo tena, akisisitiza kwamba Iran inapaswa kupanga kuingia katika orodha ya nchi 10 bora duniani katika sekta ya akili bandia.
-
Mafanikio 5 ya Iran katika Sekta ya Anga na Usafiri wa Anga kwa Kutumia Akili Bandia
Wataalamu na mafundi wa Iran wamefanikiwa kutumia akili bandia katika sekta ya anga na usafiri wa anga, hatua inayolenga kuipeleka nchi hiyo kutoka katika hatua ya uhandisi wa kubuni upya teknolojia hadi katika ubunifu wa kisasa unaotegemea akili bandia.
-
Msemaji wa IRGC: Akili bandia ilishindwa katika vita vya adui dhidi ya Iran
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Hossein Mohebi, amesema adui alitumia teknolojia za kisasa za kijeshi, akili bandia, mifumo ya uongozi na data za satelaiti na ndege zisizo na rubani katika kujaribu kuchambua uwezo wa Iran na kubaini malengo yake, lakini hatimaye ilishindwa na nguvu ya taasisi, imani, umoja, mshikamano na utashi wa wananchi wa Iran.
-
Iran Yaingia Katika Enzi ya Satelaiti Ndogo na Kubadili Ramani ya Anga za Juu
Sekta ya anga za juu ya Iran inaendelea kuhama kwa kasi kutoka hatua ya “kuthibitisha teknolojia” kuelekea hatua ya uendeshaji na mkakati, huku ikiimarisha uwezo wake katika utengenezaji na uendeshaji wa satelaiti ndogo (Mini-satellites) na mifumo ya anga za juu.
-
Iran na Iraq Zakubaliana Kuimarisha Ushirikiano wa Kisayansi na Vyuo Vikuu
Ziara ya Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran nchini Iraq imefungua njia mpya ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi, teknolojia na elimu ya juu kupitia mazungumzo na viongozi wakuu wa Iraq.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Ubunifu wa Iran umebadilisha mizani ya uwanja wa vita
Waziri wa Ulinzi na Msaada kwa Jeshi la Iran amesema kuwa katika vita vya hivi karibuni, adui alitumia teknolojia za hali ya juu zaidi duniani, lakini ubunifu na uwezo wa ndani wa Iran uliweza kubadilisha mizani ya uwanja wa vita.
-
Brigedia Jenerali Ibn al-Ridha: Vikwazo na Vita Vimekuwa Chachu ya Maendeleo ya Kiteknolojia ya Ulinzi Nchini Iran
Naibu Waziri wa Ulinzi na Msaada wa Majeshi ya Iran, Brigedia Jenerali Sayyid Majid Ibn al-Ridha, amesema vikwazo na vita vimekuwa miongoni mwa sababu zilizochochea maendeleo makubwa ya kiteknolojia katika sekta ya ulinzi ya Iran.
-
Kamanda wa Makao Makuu ya Pamoja ya Ulinzi wa Anga ya Iran: Kusasisha Uwezo na Mafunzo ni Lazima ili Kukabiliana na Maendeleo Mapya
Kamanda wa Makao Makuu ya Pamoja ya Ulinzi wa Anga nchini Iran, Brigedia Jenerali Alireza Elhami, amesema kusasisha vifaa, uwezo na mitaala ya mafunzo ni jambo la lazima ili kukabiliana na mabadiliko ya vitisho vya anga na maendeleo ya teknolojia za kijeshi.
-
Rubani wa Marekani Adai Kuona “Ndege zisizo na Rubani za Umbo la Jellyfish” Katika Anga ya Iran
Rubani wa ndege ya kivita aina ya F-15 ya Marekani amedai kuwa aliona kundi la ndege zisizo na rubani za Iran zikisafiri kwa mpangilio maalumu unaofanana na umbo la “jellyfish”, madai ambayo yamezua mjadala katika duru za kiintelijensia za Marekani kuhusu uwezo wa teknolojia ya droni za Iran.
-
Iran Yatangaza Uzinduzi wa AlphaZa, Dawa ya Kwanza ya Ndani ya Tiba ya Saratani kwa Teknolojia ya Mionzi ya Alpha
Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) limetangaza kuwa linakaribia kuzindua rasmi AlphaZa, dawa ya kwanza iliyotengenezwa nchini humo kwa kutumia teknolojia ya mionzi ya alpha, inayolenga kutibu saratani zilizo katika hatua za juu na zinazoshindikana kwa matibabu ya kawaida. Hatua hiyo inaashiria mafanikio makubwa ya Iran katika matumizi ya amani ya teknolojia ya nyuklia katika sekta ya afya.
-
Israel Yakiri Kushindwa Kukabiliana na Droni za Muqawama wa Lebanon
Jeshi la Israel limekiri kuwepo kwa hitilafu katika mifumo yake ya onyo dhidi ya droni za FPV zinazotumiwa na Muqawama wa Hezbollah, huku ripoti zikieleza kuwa teknolojia mpya ya droni hizo zinazoongozwa kwa “fiber-optic” imeongeza hofu na changamoto kubwa kwa vikosi vya utawala huo katika medani za mapambano.
-
Profesa wa Chuo Kikuu cha George Washington: Iran haiwezi kushindwa kutoka angani / Mabomu hayawezi kuangamiza maarifa na teknolojia
Sina Ozodi, Mwalimu Msaidizi wa Chuo Kikuu cha George Washington, Akosoa na Kuchambua Sera za Rais Donald Trump
-
Urusi Yatengeneza Njiwa-Droni Wenye Chipu za Ubongo
Bio-drones za Nairi Group zazua hofu za kijeshi kwa teknolojia ya udhibiti wa neva
-
Iran Yatilia Mkazo Uwezo wa Kijasusi na Kijeshi: Shambulio Lolote Litajibiwa kwa Haraka na Kwa Nguvu Kubwa
Iran imesisitiza kuwa uwezo wake wa makombora na ulinzi hauzuiliki, na shambulio lolote litapokelewa kwa majibu makali zaidi ya matarajio ya wapangaji.
-
Naibu Kamanda wa Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Iran: Hatutakuwa waanzilishi wa mashambulizi kamwe
Naibu Kamanda wa Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa jeshi halitakuwa kamwe mwanzilishi wa mashambulizi, akieleza kuwa lengo la kuimarisha jeshi sio vita, bali ni kuzuia vita na kujenga uwezo wa kuzuia (deterrence).
-
Iran yatangaza makombora yake ya masafa marefu (ICBM) yenye uwezo wa kufika hadi kilomita 10,000
Tangazo la Iran kuhusu makombora yake mapya ya masafa marefu linaonyesha ukuaji wa haraka wa teknolojia ya kijeshi ya taifa hilo na pia linaonekana kama ujumbe wa kisiasa wa onyo kwa wapinzani wake wa Magharibi.
-
Rais wa Shirika la Nishati ya Atomiki: Teknolojia ya nyuklia ni viwanda na mwanga wa afya kwa wananchi wa Iran
Rais wa Shirika la Nishati ya Atomiki ya Iran katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Mionzi kaskazini-magharibi mwa nchi, alieleza kwamba teknolojia ya nyuklia ni tasnia ya kisasa, na matumizi ya mionzi ni hatua muhimu katika kuboresha afya na usalama wa chakula nchini. Pia alisisitiza kuwa teknolojia hii inaweza kuleta baraka nyingi kwa wananchi wa Iran.
-
Iran Yazindua Makombora Mapya Yenye Uwezo wa Kuongozwa Angani
Wataalamu wa kijeshi wanaona kuwa teknolojia ya kuongozwa kwa Makombora yakiwa angani inafanya makombora hayo kuwa na faida kubwa kutokana na uwezo wake wa kurekebisha au kubadilisha mwelekeo kwa wakati halisi na Sahihi, jambo linaloongeza usahihi na kupunguza uwezekano wa kuruka hadi mbali bila kufikia shabaha yake.
-
Kibaha Dar-es-salaam | Wanafunzi wa Chuo cha Al-Mustafa Mbezi Beach washika nafasi ya pili katika Mashindano ya Kisayansi na Maarifa +Picha
Taasisi na vyuo vinne vilishiriki katika mashindano hayo, ikiwemo Taasisi ya Kimataifa ya Al-Mustafa (s). Wanafunzi wavulana wa Chuo cha Al-Mustafa - Mbezi Beach waliwakilisha taasisi yao kwa umahiri mkubwa na hatimaye wakaibuka washindi wa nafasi ya pili katika mashindano hayo.