nasaha
-
Uelewa wa Mihrabu | Nasaha 10 za Kuacha Kuswali kwa Mazoea na Kuanza Kuswali kwa Utambuzi na Unyenyekevu
Swala si kutekeleza tu rakaa kadhaa za ibada, bali ni fursa ya kuimarisha uhusiano wa mwanadamu na Mwenyezi Mungu. Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi, kupitia nasaha kumi, ameeleza adabu na mwenendo mbalimbali wa swala unaoweza kubadilisha ubora wa ibada hii. Nasaha hizo zinajumuisha umuhimu wa kuwa na uwepo wa moyo (Hudhurul-Qalb) na ikhlasi, kuswali katika wakati wake wa mwanzo, kuswali kwa jamaa, pamoja na kuswali swala za sunna (Nawafil).
-
Sheikh Ridhiwani Mjenjwa Atoa Nasaha Kuhusu Kifo kwa Akina Mama Waliohudhuria Msiba wa Muumini Mkoani Kigoma
Sheikh Ridhiwani Mjenjwa, Mudir wa Markazi ya Imam Ali (a.s) Mkoani Kigoma, ametoa nasaha kwa akina mama waliohudhuria msiba wa mmoja wa waumini katika Kijiji cha Kasuku, Barabara ya Tisa, akisisitiza kuwa kifo ni hakika isiyoepukika kwa kila Mwanadamu. Amehimiza umuhimu wa kutubu, kutekeleza wajibu kwa Mwenyezi Mungu na wanadamu, kuacha madhambi, kufanya matendo mema na kujiandaa kwa safari ya Akhera kabla mauti haijamfikia mtu.
-
Maulana Sheikh Hemed Jalala Awavisha Vilemba Wanafunzi Waliohitimu Masomo ya Miaka Mitano katika Hawzat al-Qaaim (atfs), Jijini Tanga
Zoezi la uvalishaji vilemba limeambatana na nasaha za Sheikh Hemed Jalala kwa wahitimu kuhusu wajibu wao wa kuitumikia dini, kuelimisha jamii na kuzingatia maadili ya Kiislamu baada ya kukamilisha masomo yao ya Hawza.
-
Kukumbusha upya nasaha za mwisho za Kiongozi Shahidi; Sehemu ya Nne: Simulieni nguvu na mafanikio, si udhaifu!
Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika mkutano wake wa mwisho na Rais pamoja na wajumbe wa Baraza la Mawaziri, pamoja na kutoa nasaha mbalimbali, alisisitiza mara mbili suala moja, jambo linaloonyesha umuhimu wake katika mtazamo wake: “Simulieni nguvu na mafanikio, si udhaifu!”
-
Hujjatul-Islam Tabataba’i Nejad Aeleza:
Nasaha Tatu za Imam Ja’far al-Sadiq (as) za Kulinda Dini: Kila Muislamu Ana Wajibu wa Kulinda Imani ya Familia Yake
Mhutubu katika Haram ya Bibi wa Karama (Sayyida Fatima al-Ma’suma (sa)), akizungumzia aya ya sita ya Suratul-Tahrim, alisema kuwa Mwenyezi Mungu amewaamuru waumini kwamba, kama wanavyopaswa kujitahidi kulinda dini yao wenyewe, wanapaswa pia kulinda dini na imani za familia zao. Aidha, wanapaswa kuwaamrisha watu wa familia zao kutenda mema na kuwazuia kufanya maovu.
-
Mambo Yasiyosemwa;
Kuhusu Mwenendo wa Kielimu na Kiutendaji wa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei; Sehemu ya Saba: Uteuzi wa Nasaha za Kimaadili za Kiongozi wa Mapinduzi
Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, zaidi ya kuwa mwalimu mashuhuri katika hawza za elimu ya dini, alikuwa na uhusiano wa karibu, wa kirafiki na wa unyenyekevu na wanafunzi wake. Katika mawasiliano hayo, mara kwa mara alikuwa akitoa nasaha za kimaadili kuhusu masuala mbalimbali ya mtu binafsi, familia na jamii. Kuyarejea na kuyatafakari nasaha hizo kunaweza kusaidia kufichua baadhi ya vipengele vya mwenendo wake wa kijamii na kielimu.