shughuli
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Aelekea Doha Kutoa Rambirambi Kufuatia Kifo cha Aliyekuwa Amir wa Qatar
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesafiri kwenda Doha kushiriki katika shughuli za kutoa pole na kuwasilisha salamu za rambirambi kwa viongozi wa Qatar kufuatia kifo cha aliyekuwa Amir wa nchi hiyo.
-
Kituo cha Imam Sajjad (as) Kigoma kinaendelea kuelimisha vijana na kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (as)
Chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mkuu, Sheikh Hussein Moshi Abdallah, Kituo cha Imam Sajjad (as) kilichopo Kasuko, mkoani Kigoma, kinaendelea kutoa elimu ya dini kwa vijana na kuinua bendera ya Ahlul-Bayt (as) nchini Tanzania.
-
Hali ya Majonzi Yatanda Tehran sambamba na kuanza kwa Shughuli za Kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Hali ya majonzi na huzuni kubwa imeendelea kutawala katika mji wa Tehran kuelekea shughuli za mwisho za kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei(Ra), huku umma wa Kiislamu ukiendelea kutoa heshima zake kwa Kiongozi huyu Mwema na mtetezi wa Haki za Wapalestina na Haki za wanyonge popote walipo Ulimwenguni.
-
Ratiba ya Mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran na Iraq Yatangazwa Rasmi
Msemaji wa Kamati ya Maandalizi ya Kuaga, Kusindikiza na Kuzika mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ametangaza ratiba kamili ya shughuli hizo zitakazofanyika katika miji ya Tehran, Qum, Mashhad, Najaf na Karbala. Shughuli hizo zinatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya waombolezaji kutoka Iran na mataifa mbalimbali duniani.
-
Reuters Yadai Marekani Inatafakari Kutumia Mali za Iran Zilizozuiwa Kufadhili Ukarabati wa Uharibifu katika Nchi za Kiarabu
Reuters imedai kuwa Marekani inazingatia uwezekano wa kutumia mali za Iran zilizozuiwa kufadhili ukarabati wa uharibifu wa vita katika baadhi ya nchi za Kiarabu za Ghuba.
-
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran: Bunge la Kiislamu Ni Nguzo Kuu ya Utashi wa Wananchi na Sheria
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Majlisi ya Shura ya Kiislamu ni kiini cha wananchi na nguzo muhimu ya sheria na utungaji wa sheria, akieleza kuwa taasisi hiyo ina jukumu la msingi katika kutekeleza matakwa ya wananchi ndani ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Vita Dhidi ya Iran Vyatikisa Usalama wa Chakula Sudan
Kupanda kwa bei za mafuta na mbolea kutokana na mzozo unaoongozwa na Marekani dhidi ya Iran kunatishia uzalishaji wa chakula nchini Sudan, huku zaidi ya watu milioni 19.5 wakikabiliwa na njaa kali.
-
Je, wasichana waliobalehe hivi karibuni au watu wanaopata ugumu mkubwa kufunga wanaweza kuacha kufunga?
Msichana aliyebalehe hivi karibuni au mtu yeyote anayepata ugumu wa kufunga haruhusiwi kuacha kufunga moja kwa moja kwa sababu ya hofu au dhana tu ya ugumu. Anapaswa kuweka nia ya kufunga mwanzoni mwa siku. Ikiwa wakati wa kufunga atapata taabu au mashaka makubwa yasiyovumilika, ndipo anarusiwa kufungua. Siku aliyofungua atalazimika kuilipa (qaḍā’) baada ya Ramadhani.
-
Wakala wa Mossad Akamatwa Iran Wakati wa Maandamano, Mtandao wa Ujasusi wa Mitandao ya Kijamii Wafichuliwa
Vikosi vya usalama vya Iran vimemkamata mtu anayedaiwa kuwa wakala wa Mossad wakati wa maandamano yanayoendelea, kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa ujasusi kupitia Instagram. Mamlaka zinasema mtuhumiwa ana uhusiano na shirika lenye makao yake Ujerumani, huku uchunguzi ukiendelea kubaini ukubwa wa shughuli zake.
-
Taliban Wamefunga Kituo cha Kielimu na Kitamaduni cha Imam Hussein (a.s) Jijini Kabul
Kituo cha Kielimu na Kitamaduni cha Imam Hussein (a.s) kilihesabiwa kuwa miongoni mwa vituo hai vya kitamaduni vya Waislamu wa Kishia katika magharibi mwa Kabul. Kufungwa kwake kumeibua hisia na malalamiko miongoni mwa wakazi wa eneo hilo na wanaharakati wa kitamaduni, ambao wameeleza wasiwasi wao kuhusu mustakabali wa shughuli za kielimu na kitamaduni za jamii hiyo chini ya utawala wa sasa.
-
Kongamano la Waombolezaji wa Kike wa Fatimiyyah Kufanyika Mjini Qom - Iran
Wanawake waumini jijini Qom watafanya matembezi ya maombolezo hadi kwenye kaburi la Shahidi Asiyejulikana katika chuo cha Jami‘atu-z-Zahra (a), wakiomboleza kumbukumbu ya shahada ya Bibi Fatima Zahra (a), Mama wa Maimamu wa Ahlul-Bayt (as).
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ahlul Bayt (a.s) Akutana na Imam wa Isfahan | Asisitiza Upanuzi wa Shughuli za Dini
Akizungumza kuhusu ziara yake Ispahan, Ayatullah Reza Ramadhani alikutana na Ayatullah Sayyid Yusuf Tabatabai-Nejad na kutoa ripoti kuhusu programu za mabadiliko na shughuli za kimataifa za Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s).
-
Shukrani za Ayatollah Nouri Hamadani kwa jitihada za Ofisi ya Vikundi vya Misikiti katika shughuli za Qur’an / Ihitaji uwepo mkubwa zaidi wa vijana katika Misikiti.
Kiongozi wa kiitikadi wa Mashia alisema kuwa: ‘Msikiti usio na vijana hauwezi kustawi, na uwepo wa vijana katika misikiti ni wa thamani sana.’ Alisisitiza: ‘Ninashukuru na kupongeza jitihada za Vikundi vya Utamaduni na Sanaa vya Misikiti katika shughuli za Qur’an na uhai wa misikiti, na nina matumaini uwepo wa vijana katika misikiti utakuwa mkubwa zaidi.
-
Uzinduzi wa Mfumo wa Kielelezo cha Kujadiliana na Tafsiri za Qur’ani / Ayatollah Makarem:Teknolojia Mpya Iwe Kwenye Huduma ya Qur’ani na AhlulBayt(as)
Ayatollah Makarem Shirazi, mmoja wa maraja’ wa kiislamu, akisisitiza umuhimu wa kueneza habari za mafanikio ya kisayansi, alisema: “Moja ya mahitaji muhimu ya leo ni kuwafahamisha watu. Kuna shughuli nyingi zenye thamani zinafanyika, lakini taarifa zake ni chache. Vyombo vya habari, redio, televisheni na mashirika ya habari vinapaswa kusambaza maendeleo haya ili wananchi waone kiwango cha maendeleo ya teknolojia mpya katika sekta ya elimu ya dini.”