Sheikh Hujjatul Islam wal-Muslimin Mujtaba Ashjari, Mwenyekiti wa Baraza la Uratibu wa Matangazo ya Kiislamu mkoa wa Gilan, amesema kuwa wiki ya Umoja itashuhudia mfululizo wa shughuli za kiroho, kijamii na kusaidia wahitaji, ikiwa ni pamoja na kampeni za ibada, misafara ya furaha, utoaji wa misaada kwa familia zisizojiweza, na kusaidia wanafunzi masikini.
Ismail Al-Thawabete amesema: kuomba radhi rasmi na kuanzisha uchunguzi na adui hakufuti wajibu wa kuthibitisha ukweli wala si sababu ya kutoshitaki. Uhalifu huu unahitaji kudai kufanyika kwa uchunguzi huru na wa wazi na chombo cha kimataifa kisichoegemea upande wowote, si kwa utawala wa kigaidi wa Israel.