23 Mei 2021 - 13:18
Kitendo cha Makamu wa Rais wa Marekani mkabala wa Rais wa Korea Kusini chazua gumzo katika mitandao ya kijamii

Kitendo cha Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris cha kufuta mkono wake baada ya kusalimiana na Rais wa Korea Kusini kimekosolewa sana na watumiaji wa mitandao ya kijamii na kuzusha mjadala mkubwa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Televisheni ya FOX News ya Marekani imeripoti kuwa, hatua ya Ijumaa iliyopita ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Kamala Harris,  katika mkutano wake na Rais Moon Jae-in imezua mjadala mkubwa na gumzo katika mitandao ya kijamii ambapo watumiaji wengi wa miitando hiyo wamekitambua kuwa ni kudhalilisha na kumvunjia heshima kiongozi huyo wa Korea Kusini.

Katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii, Kamala Harris alionekana akifuta mkono wake kwenye koti lake baada ya kupeana mkono na rais huyo wa Korea Kusini.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wamesema kitendo hicho ni dharau na kinamvunjia heshima Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini huku wengine wakisisitiza kuwa, lau kingelifanywa na afisa wa chama cha Republican kingekosolewa kupita kiasi. 

Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini aliwasili Washington Alkhamisi iliyopita na kukutana na mwenyeji wake wa Marekani, Joe Biden siku ya Ijumaa. 

342/