14 Oktoba 2023 - 20:00
Takwa la baadhi ya wawakilishi wa Kongresi ya Marekani la kuheshimu utawala wa Kizayuni sheria za kimataifa.

Baadhi ya wawakilishi wa Bunge la Marekani wametaka kushinikizwa utawala wa Kizayuni ili uheshimu sheria za kimataifa.

Kwa mujibu wa gazeti la Hill, wawakilishi 55 wa mrengo usiopendelea upande wowote katika Bunge la Marekani, akiwemo Pramila Jayapal, Ian Schakowsky, Mark Pukan na Jim McGovern, katika barua yao kwa Rais Joe Biden wa nchi hiyo, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken pamoja na kutaka kuwekewa mashinikizo utawala wa Tel Aviv ili uzingatie sheria za kimataifa, wamesema, wanaamini kwamba  Israel lazima itoa kipaumbele kwa mamilioni ya raia wasio na hatia huko Ghaza.Haki za wananchi madhulumu wa Palestina zimekandamizwa na utawala wa Kizayuni kwa zaidi ya miaka sabini na katika kipindi hicho utawala huo ghasibu wa Quds umefanya jinai za kutisha na kinyama zaidi dhidi ya Wapalestina Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilianzisha operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa Jumamosi, tarehe 7 Oktoba, ili kukabiliana na jinai za Wazayuni, na kushambulia maeneo yanayokaliwa kwa mabavu yakiwemo Tel Aviv, Ashdod na Ashkelon kwa mamia ya makombora na maroketi. Kufuatia operesheni hiyo kubwa, Wazayuni wasiopungua 1500 wameangamizwa. Utawala wa Kizayuni ambao umeshtushwa na kufedheheshwa katika medani ya vita na Muqawama wa Palestina katika siku chache zilizopita, umefunga vivuko vyote vya Ghaza ili kuwalazimisha wanamuqawama wa Palestina kusimamisha operesheni ya kijasiri ya Kimbunga cha al-Aqsa. Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza katika ripoti yake kwamba, idadi ya mashahidi wa mashambulizi ya mabomu ya utawala wa Kizayuni imefikia watu 1,900, ambapo 614 ni watoto na 370 ni wanawake. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu 7,696 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu ya utawala wa Kizayuni.

342/