Kuhusiana na jambo hilo serikali ya Ujerumani imetangaza kuwa imepata kibali cha awali kutoka idara husika za Wizara za Mambo ya Nje na Ulinzi za nchi hiyo cha kutuma silaha na mizinga kwa utawala haramu wa Israel.
Gazeti la Der Spiegel limenukuu duru za habari na kusema: Berlin inachunguza suala la kutuma risasi za vifaru na mizinga zinazohitajiwa na jeshi la Israel ili kuendeleza vita katika Ukanda wa Gaza na kuiunga mkono Tel Aviv katika medani zote za kikanda.
Utoaji leseni za kusafirisha zana za kijeshi za Ujerumani kwenda Israel umeongezeka mara 10 katika miezi ya hivi karibuni sambamba na kustadi mashambulizi ya utawala katili wa Israel dhidi ya Wapalestina ikilinganishwa na hapo awali, na Berlin inatoa kipaumbele sana kwa suala hilo.
Ujerumani inalipa umuhimu suala la kuiuzia silaha Israel, huku makumi ya Wapalestina wakiuawa shahidi na kujeruhiwa kila siku katika mashambulizi ya utawala huo ghasibu. Idadi ya mashahidi wa Kipalestina huko Gaza katika siku mia moja ya mashambulizi hayo imeongezeka na kufikia zaidi ya watu 24,000. Hii ni katika hali ambayo Gaza inakabiliwa na mgogoro mkubwa. Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, asilimia 15 ya wakazi wa Gaza wako katika hali ya maafa na wanasumbuliwa na njaa, na kwamba Wapalestina zaidi ya milioni moja waliolazimika kuwa wakimbizi wanaishi katika mazingira magumu.Katika hali hiyo na wakati nchi nyingi za dunia zinalaani unyama na jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Gaza, sambamba na kufanya jitihada za kukomesha mashambulizi, nkkurejesha amani na kuanda uwanja wa kufpelekwa misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina wa Gaza, nchi za Magharibi, ikiwemo Ujerumani, zinaendelea kuiunga mkono waziwazi Israel na kuruhusu kutumwa silaha na zana za kijeshi za kuendeleza maangamizi ya kizazi cha Wapalestina wa Gaza.
Hii ni pamoja na kuwa, nchi hizo za Magharibi pia zimeanza kutoa mashinikizo kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) inayoshughulikia mashtaka ya mauaji ya kimbari yaliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel. Kesi ya jinai za Israel dhidi ya watu wa Gaza ilianza kusikilizwa rasmi wiki iliyopita katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, na nchi nyingi za dunia zimeunga mkono mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya Israel. Suala hilo limezifanya nchi za Magharibi kuipatia Israel silaha zaidi, na kuzidisha uungaji mkono wao wa kisiasa kwa utawala huo. Kwa kadiri kwamba, serikali ya Ujerumani ilitangaza uungaji mkono wake kwa Tel Aviv baada tu ya kikao cha kwanza cha kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala huo haramu katika mahakama ya ICJ.
342/