Kwa mujibu wa gazeti hilo la kimataifa, Saudi Arabia na Syria, utaimarika zaidi kwa ziara ya Mrithi wa Ufalme wa Saudia Mohammed bin Salman huko Damascus na kufanya mkutano na Rais wa Syria, Bashar Assad.
Vyombo vya habari vimeongeza kuwa: Safari hiyo itafanyika katika siku za usoni na inahusiana na kumalizika vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza au kuanzishwa usitishaji vita kati ya muqawama na utawala huo. Juhudi zinafanyika ili kuhakikisha vita vya Ghaza vinasimamishwa kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Gazeti la Rai Alyoum limeendelea kusema: Iwapo safari ya mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia itafanyika huko Syria, itakuwa ni maendeleo muhimu katika uhusiano wa nchi hizo mbili za Kiarabu na itakuwa na taathira kubwa katika kurejesha uhusiano mzuri kati ya nchi nyingine za Kiarabu na Syria.
Amma kuhusu uhusiano wa Syria na Uturuki, gazeti Rai Al-Youm limeandika kuwa, uhusiano kati ya nchi hizo mbili jirani haujashuhudia maendeleo yoyote maalumu.
342/