Kwa mujibu wa Redio ya Jeshi la Israel, kikosi cha jeshi cha brigedi ya Biislamach kiliingia Rafah siku ya Jumatatu, na kuwa kikosi cha sita cha mapigano cha jeshi la Kizayuni kupelekwa katika mji huo. Redio hiyo imelielezea tangazo hilo kama kielelezo cha kupanuliwa kivitendo operesheni ya uvamizi ya jeshi la Israel huko Rafah iliyoanzishwa tarehe 6 ya mwezi huu wa Mei. Kutumwa kikosi kipya cha mapigano mjini Rafah kunafanyika licha ya amri iliyotolewa Ijumaa iliyopita na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ya kuutaka utawala wa Kizayuni usitishe mara moja mashambulizi yake katika mji huo uliofurika Wapalestina waliolazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulio ya jeshi la utawala huo.Upanuzi wa sasa wa operesheni ya kuivamia kijeshi Rafah unalifanya jeshi la Kizayuni likaribie kulidhibiti kikamilifu eneo la mpaka kati ya Ukanda wa Ghaza na Misri, linalojulikana kama Ukanda wa Philadelphia.
342/