Ali Bahraini ameyasema haya katika kikao cha 53 cha Baraza la Haki za Binadamu katika taarifa ya pamoja aliyoisoma akiziwakilishi nchi kadhaa za Kiislamu na baadhi ya nchi huru duniani.
Balozi na Mwakilishi wa Iran katika mashirika ya kimataifa yenye makao yake makuu mjini Geneva amesoma taarifa hiyo ya pamoja iliyoangazia ulazima wa kuhuisha azimio nambari 3379 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liinaloutambua Uzayuni kuwa moja ya aina za ubaguzi. Taarifa hiyo ya pamoja imeashiria ripoti ya mwaka 2017 ya Kamisheni ya Kiuchumi na Kijamii ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Magharibi mwa Asia iliyotambua Israel kuwa ni utawala wa ubaguzi wa rangi (apartheid) mkabala wa Wapalestina na kueleza kuwa: Ubaguzi wa rangi na wa aina nyingine za ubaguzi vinakiuka wazi malengo na kanuni za mkataba wa Umoja wa Mataifa. Taarifa ya pamoja ya nchi za Kiislamu na baadhi ya nchi huru duniani imeitolea wito jamii ya kimataifa kuzichukulia hatua kali taasisi za Israel zinazotenda jinai dhidi ya binadamu. Mpango huo utakuwa hatua muhimu kuelekea katika kuhuisha vifungu vikuu vya Azimio 3379 au azimio la kutambua Uzayuni kama aina ya ubaguzi wa rangi, apartheid.
342/