Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Chuo cha Al-Mustafa (s), Dar-es-Salaam – Tanzania, kimeadhimisha kumbukumbu ya Shahada ya Imam Muhammad Baqir (as) kwa kuandaa Majlis ya Maombolezo iliyojaa heshima na majonzi.
Wanafunzi wa chuo hicho walikusanyika kwa pamoja katika Majlis hiyo takatifu, wakiongozwa na Sheikh Issa Chande ambaye alikuwa khatibu wa tukio hilo. Katika hotuba yake, Sheikh Chande alielezea kwa kina maisha ya Imam Baqir (as), kuanzia utotoni mwake hadi kufikia shahada yake – akisisitiza nafasi yake ya kipekee katika kuendeleza elimu ya Ahlulbayt (as), pamoja na mazingira magumu ya kisiasa aliyoyapitia.
Hafla hiyo ilihusisha pia usomaji wa mashairi ya maombolezo, dua na ibada mbalimbali kwa ajili ya kumuenzi Imam huyo mkubwa wa tano katika mlolongo wa Maimamu wa Ahlulbayt (as).
Your Comment