Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Serikali ya Taliban imeweka vikwazo vikali vya kufanyika kwa Maja'lisi za Maombolezo za Mashia wa nchini Afghanistan ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita katika miji ya Afghanistan ambapo serikali hiyo imekataza maombolezo hayo kwa ajili ya kuadhimisha kifo cha kishahidi cha Imam Hussein (a.s), na miongoni mwa mambo waliyoyawekea vikwazo na vizuizi ni: Kuwazuia waombolezaji wa Imam Hussein kugawa nadhiri za vyakula katika barabara na miji ya Afghanistan na kuwazuia kufanya marasimu ya Maombolezo ya Shahada ya Imam Hussein (a.s) baada ya saa 10:00 (nne) kamili za Usiku.
Serikali ya Taliban imeamuru Misikiti yote ya Shia nchini Afghanistan kwamba wazungumzaji katika Misikiti hiyo wafunge Majalisi hizo za Maombolezo baada ya saa 10:00 (Nne Kamili) Usiku wakati wa Mwezi wa Muharram.
Pia, kwa mujibu wa amri hii, uundaji wa maandamano ya maombolezo ya Mashia wa Afghanistan wakati wa mchana na Usiku wa Mwezi wa Muharram hakuruhusiwi.