23 Julai 2024 - 19:32
Ripota wa Umoja wa Mataifa akosoa vitendo vya kibaguzi vya utawala wa Israel

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu huko Palestina amekosoa mienendo ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Francesca Albanese ameandika katika ujumbe wake kwenye jukwaa la X kwamba: Israel inawatendea Wapalestina kwa mfumo wa kibaguzi (apartheid), na kila siku inatumia ukatili na unyama zaidi kwa wahanga wake. 

Albanese ameongeza kuwa: Taifa la Palestina lipo, na Israel inapinga demokrasia.

Mwezi uliopita wa Juni pia Francesca Albanese, Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amekosoa vikali mauaji ya kinyama ya Wapalestina zaidi ya 200 yaliyofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kisingizio cha kuwakomboa mateka Waisraeli.Tangu kuanza kwa vita vya Gaza na uvamizi wa utawala wa Israel dhidi ya wakazi wa eneo hilo tarehe 7 Oktoba mwaka jana, karibu Wapalestina 39,000 wameuawa shahidi wengi wao wakiwa wanawake na watoto wadogo.


342/