Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA - Sheikh Qadir Akaras, Mkuu wa Umoja wa Wanavyuoni wa Ahlul_Bayt (EHLADER), alisema katika khutba za sala ya Ijumaa za wiki iliyopita katika Msikiti wa Ahlul-Bayt (a.s) Mjini Istanbul:
Wale wanaovuta pumzi kutokea Gaza na wakati huo huo hawakati mfereji wa biashara zao na utawala haram wa Kizayuni, sijui hao ni wa Dini gani!?!.
Akasema: Baadhi ya watu wanaoona dhulma hii, inakuwaje badala ya kukabiliana nayo, wanaishia (kujielekeza kwenye) kuchochea utaifa na tofauti za Kimadhehebu?!
Sheikh Akaras amesema: Leo tunaona kwamba huko Afghanistan, ISIS inawaua kikatili watu wasio na hatia mbele ya Wanawake na Watoto na kusisitiza kuwa jinai hii ilitendwa kwa sababu walikuwa ni Mashia, na picha zinazohusiana na hilo pia zinasambazwa; yako wapi mapendekezo haya katika mafundisho ya Kisunni na vipi wahalifu hawa wanajiona kuwa ni Waislamu na wanaotokana na Madhehebu ya Sunni?!