Mwandishi wa Habari wa ABNA alifanya mahojiano juu hali ya Waislamu na Mashia nchini humo (Malawi), na andiko kamili la mahojiano hayo ni kama ifuatavyo:
ABNA: Kwanza, jitambulishe.
Kwa Jina naitwa: Abdul Rashid Yusuf kutoka Malawi. Shughuli yangu kuu ni kuhubiri (Tabligh) na pia ninafundisha katika Shule (Madrasat) ya Jamiatul Mustafa (s) na Shule (Madrasat) ya Wavulana ya Pakistan. Kwa vile nilifanya kazi zaidi katika fani ya Qur'an na mimi ni msomaji na mhifadhi wa Qur'an, mara nyingi huwa ninafundisha Sayansi za Qur'an (Ulumil - Qur'an).
Pia nilikuwa na Shule iliyoitwa: "Waliyyul Asr (a.s)" ambapo niliwafundisha wahitimu wa Jamiatul Mustafa (s) na baadhi ya Masunni ambao walitaka kujua (ukweli) kuhusu Ushia. Nilifanya kazi katika Shule hii kwa muda wa miaka 5, lakini kutokana na matatizo ya kiuchumi, ilinibidi (nililazimika) kusimamisha shughuli zake. Ninatoa mfululizo wa Mafundisho (Sayansi) ya Qur'an na Maarifa ya Kiislamu kwa akina Dada wa nyumbani kwangu, ambapo sasa inajulikana kama Shule ya Mabinti miongoni mwa Mashia, na kwa sasa takriban Dada 80 wanajishughulisha na masomo hayo.
ABNA: Tuambie kuhusu matatizo ya Tabligh yako na shughuli za kitamaduni.
Tukiwa Mashia wa Malawi, tuliogopa Masunni na Mawahabi kabla ya kuanza kazi ya kuhubiri na tulikuwa na mahangaiko na wasiwasi fulani hivi, kakini tulisoma na tukaelimishwa, na tukasonga mbele katika njia hii.
Nchini Iran, nilisoma tu hadi katika ngazi ya Shahada ya kwanza (BA), na taratibu kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook na WhatsApp, hasa WhatsApp, Tabligh yetu ilipata uhai na kuimarika zaidi, kwa sababu hatukuwa na vituo vya kufanyia kazi na njia yetu pekee ilikuwa kutumia mitandao ya kijamii.
Alhamdulillah, watu wa Malawi walijifunza Mafundisho / Maarifa ya Ushia na wakashangaa kwa nini kuna mashambulizi mengi kiasi hiki dhidi ya Mashia kutoka upande wa Mawahabi?!.
Pia, baada ya mijadala tuliyofanya na wazee wa Kisunni, watu walitambua ukweli wetu na ubatili wa kauli za Kiwahabi, na sasa wanaikaribisha Shule ya Ahlul-Bayt (a.s) katika Miji tofauti, kwa namna ambayo tumeweza kuwa na Marasimu za Maombolezo ya Muharram ya Aba Abdillah al-Hussein (a.s), na programu pana juu ya maombolezo hayo katika zaidi ya Mikoa 10.
Hali hii iliwakasirisha baadhi ya watu, hivyo wakaamua / wakaazimia kuharibu bongo za watu dhidi ya Ushia kupitia njia ya kifikra na kuwasiliana na watu. Walikuwa wakidai kuwa nyinyi (yaani sisi Mashia) Serikalini si halali hivyo hamuwezi kutaka kuwa na shughuli na harakati za Kidini.
Hapo mwanzo, tulisema kwamba tuna uhuru katika dini na tunaweza kuabudu tunavyotaka. Tuliweza kupata kibali ambacho kulingana nacho Mashia wanahesabiwa kuwa ni sehemu ya Waislamu. Bila shaka, suala hili lilikubaliwa tayari, lakini kwa kibali hiki, tunakubaliwa kisheria na rasmi nchini Malawi. Pia, ikiwa Mshia yeyote nchini Malawi atakuwa na tatizo, wanaweza kurejelea Jumuiya yetu kama marejeleo rasmi.
Jina la Jumuiya yetu ni: "Jumuiya Kuu ya Ahlul_Bayt" / Ahlulbait Supreme Organization au "ASO" kwa kifupi.
Kwa hakika, taasisi zote ambazo zimekuwepo hadi leo au zitakazoundwa zitakuwa katika uwanja wetu, na muungano huu / Jumuiya hii ni Mwamvuli wa kuhami na kutoa msaada kwa Mashia na Harakati zao.
ABNA: Hali yako ya kifedha na kiuchumi ikoje?.
Naweza kusema kwamba sisi ni karibu na sifuri kiuchumi. Hata baada ya kupata leseni bado hatujui tuanzie wapi na hatuna rasilimali fedha na hata sasa hatujaweza kupata chumba wala Ofisi kwa ajili ya Jumuiya yetu.
ABNA: Je, kuna mashambulizi dhidi ya Ushia nchini Malawi kutoka kwa maadui (wa Ushia) na hata nchi za magharibi?
Nchi yetu haina unyeti uliopo katika baadhi ya nchi kama Pakistan au Iran. Kwa sababu Waislamu imma wameathiriwa na imani za Kiwahabi, ambazo zina matatizo kati yao wenyewe, au kwa sababu hawajui hasa hali ya Kimadhehebu ikoje. Kwa hiyo hii ni fursa kwetu sisi kuwavutia kwa urahisi kwa kuieleza Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s).
Kwa hiyo, ikiwa kuna tatizo, ni kutoka ndani ya nchi na hakuna mashambulizi kutoka nje dhidi yetu.
Bila shaka, Mawahabi wanaungwa mkono na Saudi Arabia, wana Idhaa za Redio na Televisheni, na wanafanya Shughuli / Harakati nyingi sana.
Ikiwa tutakuwa na uwezo tu wa kufanya harakati kwa Mazungumzo na Tabligh kwa maneno, na ikiwa pia tutakuwa na vifaa na media pana, basi tunaweza kuwa na ufanisi zaidi (katika Harakati za Kitabligh), kwa kuzingatia kuwa kuna upatikanaji wa jukwaa pana (la kitabligh).