21 Desemba 2024 - 05:36
Bendera ya Israel yashushwa katika jengo la ubalozi wa Israel Dublin

Bendera ya utawala haramu wa Israel imeshushwa na kuondolewa katika jengo la ubalozi wa Israel mjini Dublin Ireland baada ya ubalozi wa utawala huo kufungwa.

Ireland ni miongoni mwa mataifa ya Ulaya ambayo yamekuwa yakishuhudia maandamano makubwa ya kulaani jinai za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Aidha serikali ya Ireland imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono Wapalaestina ana kupinga jinai za Israel dhidi ya Wapalestina.

Jumapili iliyopita Gideon Sa'ar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala wa Kizayuni alitangaza kufunga ubalozi wa Tel Aviv nchini Ireland kutokana na kile alichokiita kuwa eti "sera za Ireland dhidi ya Israel".

Baada ya hhatua hiyo serikali ya Ireland imetangaza kuwa, Israel haina uwezo wa kuzima sauti ya Wa-Ireland ya kuwaunga mkono Wapalestina.

Waziri Mkuu wa Ireland Simon Harris amesema kuwa, nchi yake itaendelea kukosoa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na kwamba utawala huo hautaweza kuzima sauti ya Ireland.

Aidha hivi karibuni Waziri Mkuu wa Ireland alisisitiza kuwa, nchi yake itatekeleza amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuhusu kukamatwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Yoav Gallant Waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

parstoday